Mkuu wa Mradi wa VASPHARD Dk. Faith Mabiki akizungumza kwenye mafunzo kwa Waganga wa Tiba Asili   ya siku moja ya watengenzaji wa dawa za asili kutoka mikoa mbalimbali yaliyofanyika mkoani Morogoro jana

Mhadhiri wa  Idara ya Sayansi ya mazao ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Dk. Richard Madege akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa.

Mafunzo yakiendelea.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.

Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa.

Taswira ya mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.

Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa.

Madawa yakiwa yamehifadhiwa kwenye boksi wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo hayo.
 


Na Calvin  Gwabara,  Morogoro.


CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kupitia mradi wa VaSPHARD kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wamefanya  mafunzo kwa Waganga wa tiba asili na kisha kupima dawa zao ili waweze kubadilisha mtazamo na tabia  katika kuzalisha dawa kutakakopelekea  waweze kutengenza dawa salama,safi na zenye viwango vya juu na kupata usajili.

Akizungumza na SUA MEDIA Mkuu wa Mradi wa VaSPHARD Dk. Faith Mabiki alisema kuwa mafunzo hayo yanawakutanisha waganga wa tiba asili na watengenezaji wa dawa zaidi ya 35 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ambao wamekuja na dawa zao zaidi ya 100 ambazo baada ya majadiliano na kujengeana uelewa wa zoezi hilo zitapimwa na kisha kupewa majibu kujua ubora wa dawa hizo na kuwashauri namna bora za kuzalisha na kufungasha dawa zao kukidhi viwango vya kimataifa.

“Kwa hiyo sasa hivi tunajadiliana nao baada ya kuwajengea uelewa na tunaingia nao makubaliano kisha tutakwenda maabara kufanya vipimo viwili ambavyo vimewekwa na serikali ili waweze kutengeneza dawa kiusalama zaidi”. alieleza Dk. Mabiki.

Aliongeza “Ili Serikali iweze kuzitangaza dawa hizo lazima wapelekwe kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuangaliwa vipimo kadhaa kama vile sumu kuvu,vipimo vya wadudu wanaosababisha magonjwa au dawa kuwa chafu, vipimo vya madini tembo  na Kemikali iliyo ndani ya dawa hizo, na kwa bahati nzuri vipimo hivyo vyote SUA tunaweza kuvifanya ndio maana mkemia mkuu wa Serikali ametupa kufanya baada ya kupata hela kidogo kutoka kwa Jumuiya ya wanataaluma wa Sayansi Afrika tunakwenda kufanya kazi hii”.

Alisemaa kama kweli Taifa linataka kuona Dawa wanazotengeneza zinachangia afya ya Jamii na maisha ya wataalamu hao wa tiba asili lazima swala la ubora wa dawa hizo lizingatiwe hapo ndipo wataweza kulifikia soko kubwa la ndani ya Tanzania na nje kama ambavyo nchi zingine maarufu kwa uzalishaji wa dawa hizo wamefikia mfano India na China.

Dkt.Mabiki amesema kuwa zoezi la upimaji wa dawa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali lina gharama kubwa kama ambavyo waganga hao wamesema lakini SUA kama taasisi ya Elimu na Utafiti wanavyo vifaa vya kisasa na bora lakini pia wanao wanafunzi wanaofanya tafiti hizo kwenye shahada mbalimbali za Juu ambao wanatumia dawa hizo kuzifanyia utafiti na kupata shahada zao lakini pia waganga wenyewe wenye hizo dawa wanapata kupimiwa dawa zao bure na kupewa ushauri wa namna ya kufanya na kisha kuweza kupata usajili baada ya kukidhi vigezo vya Serikali.

“Kwahiyo hapo tunatengeneza muunganiko mzuri kati ya watafiti, Waganga wa tiba asili na viwanda maana hawa ukiwangaalia kazi zao ni viwanda tena vya muhimu sana hasa ukiangalia jinsi sekta hii ya tiba asili inavyokuwa kwa kasi na kuingiza fedha nyingi duniani na sisi tunataka kama Chuo na Taifa kuona wataalamu hawa wa tiba asili wanatengeneza pesa nyingi na kuboresha Maisha yao na kuchangia pato la taifa” alisistiza Dk. Mabiki.

Mkuu huyo wa mradi wa VaSPHARD alisema mafunzo hayo ni muendelezo na mafunzo mengine mbalimbali ambayo yamefanyika huku nyuma lakini pia ni kutokana na tafiti walizozifanya na kubaini kuwa zipo changamoto kwenye uzalishaji wa dawa hizo lakini watengenezaji hao hawazijui hasa baada ya kuchukua dawa kadhaa huko nyuma na kuzipima na kugundua kuwa ni chafu lakini baada ya kuwaeleza na kuwashauri namna nzuri ya utengenezaji wa dawa hizo wakaenda kutengeneza na kurudisha dawa hizo zikiwa safi.

Kwa upande wake Mtaalamu wa tiba asili kutoka Njombe, Flavian Nyakeji alisema amefurahi kupata nafasi hiyo ya kipekee ya kuelimishwa na kujua namna ya kutengeneza dawa zenye ubora anazizo na madhara kwa wateja na watumiaji wao kwa ujumla.

“SUA imetusaidia kwa muda mrefu kuboresha utengenezaji wa dawa zetu wanataka tufikie viwango vya juu, na sisi hili ndilo tunalolitaka maana sisi tunaotoka Njombe tunauza Njombe tuu, linini tutauza Dar es salaamu,lini tutauza Mwanza?, Lini tutauza Kenya? lini tutauza Ulaya na hii ilitokana na kutengenza kwa Viwango vya chini lakini sasa tunashukuru Mungu amewanyanyua wataalamu wa SUA sasa wametengenza nyororo ambao kuna watu wamesoma lakini hawajafanya kwa vitendo na sisi ambao hatujasoma lakini tunafanya kwa vitendo na kupitia kwao sasa tunaneemeka maan masoko wanayajua” alisema  Nyakeji.

Nyakeji amesema ameleta dawa kumi kwenye zoezi hilo ili aweze kujua nini kipo kwenye dawa zake hasa kwa kujua ubora wake na yupo tayari kupata ushauri wa kitaalamu wa namna ya kuboresha dawa hizo ili ziweze kuwa na viwango badala ya kuzalisha bila viwango hali ambayo itatunyima usajili na kutofikia soko la nje.

Mtaalamu huyo wa Tiba asili amesema kupitia mafunzo na uwezeshwaji huo wa kitaalamu tayari kuna mabadiliko makubwa kati uzalishaji wa tiba asili nchini na anaamini kuwa kutafanyika mapinduzi makubwa katika soko la tiba asili nchini na wataweza kuuza bidhaa zao nchi ya nchi kama ambavyo nchi zingine zinauza Tanzania.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: