Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omari Kipanga (Mb) amekamilisha ziara yake ya siku tatu mkoani Dodoma kwa kukagua maendeleo ya awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara hiyo iliyopo eneo la Mtumba Jijini Dodoma.


Mhe. Kipanga ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi na kumtaka mkandarasi wa ujenzi huo, kampuni ya CRJE (EA) Limited  kuhakikisha wanatekeleza ujenzi huo kwa kiwango na  kukamilisha kwa wakati uliopangwa.


Aidha amefafanua kuwa ujenzi wa jengo hilo utagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 15.9 na kwamba jengo litakuwa na sakafu nane ikiwemo sakafu ya ardhini (basement), sakafu ya chini (ground floor) na sakafu za juu sita.


Akitoa ripoti ya mradi huo, Mkadiriaji Majenzi kutoka Chuo cha Ardhi ambao ndio wasimamizi elekezi wa Mradi, Anania Saudeni amesema ujenzi wa jengo hilo ulianza Desemba 2021 na unatarajia kukamilika Desemba 2023 na kwamba mpaka sasa umefikia asilimia tano.


Naye Meneja wa Mradi huo, Li Yang ameihakikishia Wizara hiyo kukamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa na kwa kiwango kinachotarajiwa.

Share To:

Post A Comment: