MTAFITI Mwandamizi kutoka Taasisi inayojihusisha na Tafiti katika Nyanja za Uchumi na Jamii (ESRF) Vivian Kazi akizungumza wakati wa kikao hicho

Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) Morogoro Dk Winifred Mbungu akizungumza
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatilia kwa umakini
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatilia kwa umakini
NA OSCAR ASSENGA,TANGA


MTAFITI Mwandamizi kutoka Taasisi inayojihusisha na Tafiti katika Nyanja za Uchumi na Jamii (ESRF) Vivian Kazi ameishauri Serikali kuona namna nzuri ya kuweza kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuhakikisha wakulima wanalima kilimo kinachostahimili ukame

Vivian aliyasema hayo wakati wa kikao chao cha kuwasilisha utafiti ambao ulifanywa na Taasisi hiyo na Chuo Kikuu cha Sokoine Morogoro (SUA) kwa awamu mbili mwaka 2019 na 2021 lengo kubwa wamechagua Tanga kama eneo lenye sifa ya hali ya hewa inayowakilisha maeneo mengi nchini hali ya hewa nzuri kwenye nyanda za juu na chini   

Vivian ambaye pia ni  Mkuu wa Idara inayojihusisha na tafiti za kimkakati na machapisho na ESFR kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Leeds,Abadin vya Uingereza,Sua na Chuo cha Ku cha Nelson Mandara Arusha wamekuwa wakifanya kazi ya mradi unaojihusisha na mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Mradi huo wa miaka minne umefanyika na mapendekezo waliyoyatoa ni kuweza kulima kilimo stahimilivu na mabadiliko ya tabia ya nchi kuweza kutumia teknolojia ya chini au kati ili kuongeza kilimo tija na kuweza kulima mazao ambayo yataweza kustahimili mabadiliko ya tabia ya nchi.

Akizungumzia athari za mabadililo ya nchi,Vivian alisema mabadiliko ya tabia ya nchi yameathiri nchi nyingi tajiri na masiki ikiwemo kuathiri kwa kiasi kikubwa mabadilko ya mvua hatua ambayo inasababisha mazao kutokuua kwa wingi wakati wa mavuno.

 “Kwenye tafiti zenu tuliliona hilo na ifikapo mwaka 2050 kama zisipochukuliwa juhudi za makusudi athari zitakuwa kubwa kiasi huku wakishauri hatua zianze kuchukuliwa mapema kuweza kukabiliana nazo”Alisema

Alisema lengo la mkoa wa Tanga kuwepo miongoni mwa mikoa kwenye mradi huo unaojihusisha na mabadiliko ya tabia ya nchi kilimo stamilivu na usalama wa chakula kwa Tanzania kutokana na kuwa eneo lenye sifa ya hali ya hewa inayoweza kuwakilisha maeneo mengi nchini na kuna mpango wa kuongeza uwezo maafisa kilimo,maafisa ugavi.

Aidha alisema mradi huo ambao ulianza mwaka 2018 ambao ni wa miaka minne una lengo la mradi kushauri kwenye mambo ya sera kitu gani kifanyike kwa Tanzania kuhakikisha wanapambana na mabadiliko hayo ya tabia ya nchi.

Aliongeza namna ya kukabiliana nao ni kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwa wakulima kulima kilimo stamilivu na kuangalia mazao yanayostahimili mabadilio hayo pamoja na usalama wa chakul,lishe na biashara kama watapata satras.

“Lakini kuna mafanikio mengi kwenye mradi mpango wa kuongeza uwezo maafisa kilimo,maafisa ugavi ,watafiti na wamefanya tafiti kwenye sera kwa kuhojiana na wadau mbalimbali  katika ngazi za wizara na ngazi za idara serikali na wakala mbalimbali”Alisema  

Hata hivyo aliwataka maafisa ugani mkoani Tanga kutumia vema elimu waliopewa  na taasisi hiyo ili kuweza kuwasaidia wakulima kuweza kulima kwa tija na kuondokana na kulima kimazoea ambapo wakati mwengine wanakosa mavuno.

Vivian aliyasema hayo wakati walikuwa na mkutano wao na watafiti na maafisa kilimo kutoka wilaya ya Muheza na Lushoto zilizopo mkoani Tanga kuweza kuwasilisha utafiti ambao

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) Morogoro Dk Winifred Mbungu  alisema ameshiriki kwenye utafiti na watalamu mwengine kutoka nchi za Afrika ambazo ni Malawi ,Zambia,Afrika Kusini na Tanzania  yeye pamoja na wengine wameshiriki kujaribu kuona mkusanyiko kufanya utafiti kwa ajili ya kuangalia athari diet na gesi.

Alisema katika utafiti huo ulikuwa shirikishi wao kama nchi walikwa wanaangalia wanapokwenda na kuangalia namna gani wanaweza kustahimili mabadiliko walilenga miaka 2050 ambapo mabadiliko yanatokea na maendelea yanatokokea.

Alisema miaka 2050 inakadiriwa joto linatarajiwa kuongezeka na linakwenda kuathiri mazao hasa ya wanayozalishwa lakini zao hilimilivu ni soya ambalo linaweza kuthimili na kwa Tanzania wana watu wanaokadiriwa milioni 60 na kwa mwaka 2050 inakadiriwa kutakuwa na watu milioni 100 sasa wanatakiwa wawe wanazalisha chakula ardhi hiyo hiyo hawataweza kwenda mbele kama hawatutaingiza teknolojia.

Kwa upande wake Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Emigidius Kasunzu aliwataka maofisa kilimo kutumia elimu waliyoipata kuwaelekeza wakulima kulima mazao yanayohimili hali ya ukame .

Aliwataka wataalamu wa kilimo na waatafiti kufanya utafiti na ugunduzi wa mbegu bora pamoja na tekinolojia ya kisasa ili wakulima waweze kuwasaidia  kulima kulima kilimo chenye tija. 

" Uvunaji wa maji utunzaji wa mazinhira pamoja na upatikanaji wa mbegu bora utaweza kutusaidtia kujiepusha na baa la njaa kwa siku za mbeleni ' Amebainisha Kasunzu 


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: