Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha TLP, Augostino Mrema akifunga ndoa na Doreen Kimbi.


Na Thobias Mwanakatwe, Moshi


MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha TLP, Augostino Mrema, amesema anamshukru Mungu kwa sherehe ya ndoa yao kwenda vizuri na kwamba wanaoendelea kueneza uzushi na upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii wanapoteza muda wao.

Akizungumza na gazeti hili alisema anamshukru Mungu kwasababu taratibu zote za ndoa zilifuatwa hivyo mke wake Doreen Kimbi hajamuoa kinyemela.

Mrema alisema ndoa yake awali nilikuwa ifanyike Machi 8 mwaka huu lakini waliamua kuisogeza mbele hadi Machi 24 ili kutoa fursa kama kulikuwa na mtu ambaye angejitokeza kuweka pingamizi ndoa isiweze kufungwa.

" Ndoa imetangazwa kanisani mara tatu na hakuna mtu yeyote aliyejiyokeza kusema Doreen alikuwa mke wangu kwa hiyo uvumi wa mitandaoni hauna maana yeyote na wanaofanya hivyo wanadhani watavuruga ndoa yetu kumbe wanapoteza muda wao bure," alisema Mrema.

Alisema hadi kufikia Machi 23, mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya kufungwa kwa ndoa hiyo hakuna mtu yeyote aliyejitokeza kutoa pingamizi hivyo wanaoeneza uvumi mbalimbali kwenye mitandao wanapoteza muda wao ndoa imeshafungwa na hivyo suala hill limeshapita.

 Mrema alisema uvumi wa mambo yote hayo unatokana na kwamba watu hawajazoea mtu akipendwa kwa dhati na mtu mwingine,watu wamezoea rushwa wanahonga watu,wananunua watu,kwa hiyo wanafikiri kila mtu ananunulika.

Alisema mara baada ya mke wake kufariki Septemba mwaka jana, alimuacha katika mazingira magumu sana hivyo alimuomba Mungu amsaidie ili apate msaidizi mwingine.

"Mke wangu alipofariki aliniacha katika mazingira magumu sana afya ilikuwa imedorora hata hotuba yangu wakati wa kumzika sikuweza kusimama, nilimuomba Mungu na mke wangu atakapokuwa anisaidie nipate mtu atakayenitunza, atakayeniangalia," alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na maombi yake hayo baraka za mwenyezi Mungu zilikuja na ndipo akajitokeza huyo binti (Doreen) akakubali kutumia maisha yake kwa ajili ya kunitunza.


 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: