Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC) kilichoketi mjini hapa leo..

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akitoa mpango mkakati wa kuinua elimu katika kikao hicho.

Wakuu wa Wilaya za Singida wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Jerry Muro (Ikungi) Mhandisi Paskas Muragili (Singida Mjini) Sophia Kizigo (Mkalama) na Suleiman Mwenda (Iramba)

Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu wa Mkoa wa Singida,  Beatrice Mwinuka akitoa taarifa katika kikao hicho. 
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Jumanne Mlagaza, akielezea kuhusu utekelezaji wa mpango wa Anwani za Makazi na Postikodi.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini Mhandisi Paskas Muragili akielezea kuhusu uchakavu wa magari ya polisi, nyumba ya DC na uendelezajiwa mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Kiijiji cha Kisasida uliopo Manispaa ya Singida.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu akizungumzia umuhimu wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwenye kikao hicho.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akichangia jambo kwenye kikao hicho.



Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumza kwenye kikao hicho ambapo aliomba kupatiwa gari baada ya analolitumia kuharibika mara kwa mara hivyo kuwa na changamoto wakti wa utekelezaji wa majukumu yake.

Wawakilishi wa wabunge wa Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Baadhi ya viongozi na wakuu wa idara wakiwa kwenye kikao hicho.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga na Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu wakiwa kwenye kikao hicho.

Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Hussein Simba (Itigi) James Mkwega (Mkalama) Eliya Digha (Singida DC) na Jumanne Mlagaza.

Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya za Singida wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Ester Chaula (Singida DC) John Mgalula (Itigi) Justice Kijazi (Ikungi)  Melkizedeck Humbe .(Manyoni) na Asia Mesos (Mkalama)
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Watumishi wa Umma kutoka idara mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Winfrida Funto akipitia kabrasha lenye taarifa ya kikao hicho.
Kikao kikiendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Taswira ya kikao hicho.
Katibu Tawala Msaidi upande wa Uchumi na Uzalishaji Beatus Choaji akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega akichangia jambo kuhusu mpango wa Anwani za Makazi na Postikodi.

Kikao kikiendelea. Kushoto ni Katibu wa Mbunge wa Ikungi Mashariki, Ally Rehani  na kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Mjini Shabani Karage.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Manzingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Said akitoa taarifa ya miradi ya maji inayotekelezwa mkoani hapa.
Meneja wa   Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Singida, Lambert Bayona akizungumza kwa niaba ya Meneja wa mkoa huo kuhusu ujenzi wa barabara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Eliya Digha akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe akitoa taarifa kuhusu Anwani za Makazi na Postikodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Ester Chaula akitoa taarifa kuhusu mpango wa Anwani za Makazi na Postikodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Michael Matorora akitoa taarifa ya mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Mesos akitoa taarifa kuhusu mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi  John Mgalula akitoa taarifa ya mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni  Melkizedeck Humbe .akitoa taarifa kuhusu Anwani za Makazi na Postikodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi akitoa taarifa hiyo.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida

KATIKA mwaka wa fedha 2022/23 Mkoa wa Singida umekadiria kutumia Sh. 261,012,288,000 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo ambapo Sh. 189,766,303,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida (Mishahara na Matumizi  Mengineyo) Sh.  71,245,985,000 ni kwa miradi ya maendeleo.

Hayo yalisemwa na Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu wa Mkoa wa Singida,  Beatrice Mwinuka wakati akitoa taarifa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC) kilichoketi leo mjini hapa.

Alisema kwa matumizi ya  kawaida, Sh.  164,619,385,000 ni mishahara na Sh. 25,146,918,000 ni matumizi mengineyo.

Mwinuka alisema  miradi ya maendeleo, Sh. 29,454,898,000 zinatokana na fedha za ndani na Sh. 41,791,087,000 ni fedha za nje.

Alisema kwa Sekretarieti  ya Mkoa, Sh. 5,020,614,000 ni matumizi ya kawaida na kuwa  Sh. 2,789,904,000 ni mishahara na Sh. 2,230,710,000 ni matumizi Mengineyo.

Alisema katika mwaka 2022/23, Mkoa umekadiria kukusanya jumla ya Sh. 18,274,735,000  kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani (Own Sources) ikiwemo Mapato halisi (Own Source Proper) Sh. 14,181,147,000 na Mapato lindwa Sh. 4,093,588,000.

Alisema kati ya fedha zitakazokusanywa kutoka mapato halisi, kiasi cha Sh. 5,672,458,800 zitatumika katika shughuli za Maendeleo na Sh. 12,602,276,200 zitatumika kugharamia Matumizi ya Kawaida.

Alisema Mkoa wa Singida unaomba kuidhinishiwa jumla ya Sh., 261,012,288,000. Kati ya hizo Sh. 18,274,735,000 ni makusanyo ya ndani, Sh. 164,619,385,000 ni kwa ajili ya Mishahara,Sh.i 25,146,918,000 kwa ajili ya matumizi mengineyo  Sh. 71,245,985,000 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo .

Aliongeza kuwa katika bajeti inayoandaliwa, fungu huwekewa ukomo wa bajeti, ikiwa ni fedha za ndani kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Pamoja na ukomo kutolewa bado kuna uhitaji mkubwa, mkoa utawasilisha maombi maalum yenye Jumla ya Sh.18,947,827,950.00 kwa ajili ya kuboresha ufanisi na kuongeza tija na maendeleo katika Mkoa wa Singida.

Akizungumzia kuhusu suala la Anwani za Makazi na Postikodi Mwinuka alisema Halmashauri zimetoa mafunzo kwa Waheshimiwa Madiwani wote, Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata na Watendaji wa vijiji wote.

Alisema Halmashauri zimefanikiwa kutambua taarifa za majina ya barabara, mitaa/vitongoji. Halmashuri ya Wilaya ya Mkalama, Manispaa, Manyoni na Ikungi. zimeshawasilisha makadirio ya Anwani ya makazi kwa Mratibu wa Mkoa na tayari zimeshatoa matangazo ya ajira ya muda na kufanya usaili.

Akizungumzia mpango wa matengenezo ya barabara  kwa  mwaka 2022/ 2023 kwa kila halmashauri kwa niaba ya Meneja wa   Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Singida Meneja wa TARURA Manispaa ya Singida, Lambert Bayona alisema fedha zilizotengwa  kutoka katika mfuko wa barabara  kwa Manispaa ya  Singida ni 1,248,630,00, maendeleo ya jimbo 500,000,000 na nyongeza bajeti na tozo ya mafuta ni Sh.500,000,000.

Alisema kwa  Singida DC kutoka mfuko wa barabara ni Sh.668,030,000, maendeleo ya jimbo Sh.500,000,000 na nyongeza bajeti tozo ya mafuta, 1,000,000,000.

Kwa Ikungi fedha zilizotolewa kupitia mfuko wa barabara ni 881,040,000, maendeleo ya jimbo, Sh.1,000,000,000 na nyongeza ya bajeti tozo ya mafuta ni Sh. 2,000,000,000.

Alisema kwa wilaya ya Manyoni fedha kutoka mfuko wa barabara ni Sh. 706, 570,000, maendeleo ya jimbo  Sh.500,000,000 na nyongeza ya bajeti tozo ya mafuta 1,000,000,000.

Iramba fedha za mfuko wa barabara ni Sh.824,920,000, maendeleo ya jimbo 500,000,000 na nyongeza ya bajeti tozo ya mafuta ni Sh.3,000,000,000 na Mkalama  fedha za mfuko wa barabara ni Sh.658,840,000, maendeleo ya jimbo Sh. 500,000,000 na nyongeza ya bajeti na tozo ya mafuta ni Sh.1,000,000,000.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka  2021/2022 Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Manzingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Said alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 mpaka kufikia februari  2022 kazi ambazo  zimetekelezwa ni  utafutaji wa vyanzo vipya vya maji na kupima ubora wa maji ya vyanzo hivyo.

Alisema katika kipindi hicho  jumla visima virefu 26 vimechibwa kwa gharama ya Sh. 647,978,672 Ikungi  kimoja kwa gharama ya Sh.36,639,, Iramba 18 kwa gharama ya Sh.350,145,400, Manyoni viwili kwa gharama ya 89,145,400, Mkalama 4 kwa gharama ya Sh. 136,833,272 na Singida DC kimoja kwa gharama ya Sh.36,639,000 huku jumla yake ikiwa ni Sh.649,256,672.

Saidi alisema  katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 jumla Sh. 13,676,856,941. zilitengwa kw ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji na mpaka kufikia 28 februali. 2022, jumla Sh. 6,168,609,857 zimeshapokelewa sawa na 45% ya fedha zote.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko akizungumzia mpango mkakati waliouwekwa wa kukuza taaluma mashuleni hasa shule za msingi alisema wamepanga kuboresha Mahudhurio ya Walimu na Wanafunzi ,Mazingira Rafiki kwa walimu na wanafunzi kuwa shuleni wakati wote wa masomo kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 8.30 mchana ,kukamilisha Miundombinu ,kutoa chakula ,kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi  na kutoa huduma za bweni.

Mwaluko alisema mkakati mwingine walioupanga ni kuanza kutoa elimu kwa njia ya TEHAMA jambo litakalo saidia  kuwafundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja hasa kwenye zile shule ambazo zinawafunzi zaidi ya 400 lakini wanafundishwa na mwalimu mmoja kutokana na Yule husika kutokuwa na walimu.

Alitaja malengo mkakati mengine kuwa ni kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo yote, masomo yote kufundishwa hata kama hakuna mwalimu katika shule,  kuajiri walimu wa kudumu na kujitolea, kuimarisha uwezo wa walimu kitaaluma, kukuza matumizi ya TEHAMA,kuhakikisha uwepo wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ,kusawazisha mtawanyo wa Walimu na Kutoa masomo katika Muda wa ziada.

Mwaluko aliutaja mpango  mkakati wa tatu kuwa ni kuimarisha Uwajibikaji na Ushiriki,kuboresha uwajibikaji wa wasimamizi, jamii na wanafunzi,kuimarisha uwezo wa wasimamizi wa elimu ngazi zote, kusimamia nidhamu, wajibu na haki za walimu, kutoa elimu ya malezi na makuzi kwa wanafunzi  na kutoa elimu kwa jamii.


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: