Afisa Viwango TBS, Bw.Henry Massawe akizungumza na waandiishi wa habari leo katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es salaam.

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIKA kuelekea Siku ya Viwango Afrika, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepanga kukutana na wadau ili kujadiliana ushiriki wao katika shughuli za uandaaji wa Viwango ambapo itafanyika kwenye ofisi za TBS Kanda Mkoa wa Arusha tarehe 29 hadi 31 Machi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Afisa Viwango TBS, Bw.Henry Massawe amesema wameandaa mkutano wa wadau wa sekta ya Utalii kufanya majadiliano kuona mchango wa viwango ukitumika vizuri katika kukuza sektarisch hio. Pia maeneo gani ambayo yanaonekana yanauhitaji wa Viwango.

Amesema watawakutanisha pia wadau wa umeme na kutoa elimu katika Viwango vya nyaya za Umeme hususani katika eneo la mabadiliko ya rangi za nyaya za umeme, kumetokea mabadiliko katika viwango rangi za nyaya za umeme lakini utekelezaji wake umekuwa na changamoto hivyo ni fursa pekee kwa wadau wa Umeme kushiriki na kujadiliana njia bora ya utekelezaji wa Viwango husika.

"Tutawakutanisha watueleze ni changamoto gani ipo lakini maeneo gani kama TBS tunahitaji kufanya viwango tuwekeze huko". Amesema Bw.Massawe.

Aidha Bw.Massawe amesema tarehe 31, Machi 2022 ambapo maadhimisho hayo yatakuwa tamati kwa Tanzania, watakuwa na na kutaoneshwa kwa vitendo moja ya utaratibu wa kuandaa Viwango kupitia kamati za kitaalamu. Kamati ya kitaalamu itakuwa na Kikao na namna ya majadiliano ya kuandaa Viwango vya kitaifa na wageni waalikwa watakuwa kama wafuatiliaji.

Ameeleza kuwa siku hiyo kutakuwa na tukio maalumu la ugawaji zawadi kwa washindi wa shindano la uandishi wa Isha kwa wanafunzi wa elimu ya Juu, shindano ambalo lilianza Rasmi Novemba 25 , 2021 ambapo isha 223 zilipokelewa.

"Tumesahihisha hizi Isha 223 tukapata isha bora 10 ambapo wameeleza vizuri mchango wa Viwango katika kutatua changamoto mbalimbali za magonjwa ya milipuko, insha zimeeleza vizuri, viwango ni nini, changamoto mbalimbali ambazo zililikumba bara la Afrika katika kuagiza vifaa tiba na madawa katika kupambana na UVIKO -19 ". Amesema
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: