Kamati  ya  Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LACC)  imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa  Ofisi ya Utawala ya Halmashauri ya   Wilaya  ya Mbeya.


Pia  imemtaka  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Stephene Katemba kuendelea kusimamia na kufanya tahmini ya  matumizi ya fedha  katika kila hatua ya utekelezaji.


Akizungumza 21, Machi, 2022, Kaimu Mwenyekiti  Mhe. Boniface Butondo amesema baada ya kukagua ujenzi huo kamati imeridhishwa na  matumizi ya fedha ukilinganisha  na hatua ya utekelezaji  iliyofikiwa.

Pamoja na pongezi hizo  Mhe. Butondo amewashukuru wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya   kwa kushiriki katika  uchimbaji wa msingi hatua ambayo imeokoa Sh milioni 1.7.


" Niwashukuru wananchi kwa kuchangia nguvu kazi na niwaombe muendelee na ari hiyo kwa miradi mingine ya maendeleo ili kupunguza gharama za ujenzi."


Kwa upande wake Mhe.  Francis Mtinga mbaye ni mjumbe wa Kamati  amempongeza Mkurugenzi kwa   kununua  mashine kwa ajili ya kufyatulia tofali na mashine ya kuchanganyia zege vifaa ambavyo vitasaidia kupungiza gharama za miradi na zitatumia kwa miradi mingine ya maendeleo.


Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya. Bw Stephene Katemba amesema hadi kukamilika ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya utagharimu kiasi cha Sh 2,792,073,029.88 kati ya hizo Sh 2,700,000,000 ni fedha za ruzuku kutoka Serikali Kuu na Sh 92,073,029.88  zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.


Aidha amemshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa jengo ambao umelenga kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma








.

Share To:

Post A Comment: