Na Englibert Kayombo - Geita.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Kifua Kikuu imetoa rai kwa Makampuni ya Migodi kuwa na mpango endelevu wa kutoa elimu ya kujingina na magonjwa ya UKIMWI na Kifua Kikuu kwa wafanyakazi. 


Rai hiyo imetolewa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Hassan Toufiq mara baada ya Kamati kutembelea Mgodi wa Geita kuona utekelezaji wa afua mbalimbali za kupambana na UKIMWI na Kifua Kikuu. 


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Kifua Kikuu imeupongeza Mgodi wa Geita (Geita Gold Mine) kwa kutoa elimu ya Masuala ya Ukimwi na Kifua Kikuu kazini.


"Hapa tumeona mnafanya vizuri katika kutoa elimu ya kujilinda dhidi ya magonjwa ya UKIMWI na Kifua Kikuu, hongereni sana na sehemu nyingine pia wafanye hivi ikiwa ni pamoja na kuwatunza watu wanaoishi na UKIMWI na Kifua Kikuu" amesema Mhe. Toufiq


Mhe. Toufiq amesema sehemu za Migodini huwa na watu wengi wanaopata maambukizi ya Kifua Kikuu kutokana na mazingira wanayofanyia kazi kuwa na vumbi jingi na kuitaka Migodi kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi ili kujiepusha na Ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Share To:

Post A Comment: