Chuo cha Uhasibu Arusha IAA kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kupitia  chuo cha mafunzo ya maafisa wa kijeshi Monduli TMA wametiliana Saini makubaliano ya kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu ya utafiti na ushauri katika fani mbalimbali zinazotolewa na chou hicho kwa maafisi wa Jeshi hilo. 


 Akizungumza wakati wakitiliana saini kwenye Chuo cha Uhasibu Arusha Kaimu Mkuu wa chuo cha Uhasibu Dkt.Cairo Mwaitete Amesema kwamba mkataba huo utaleta mafaniko baini ya Taasisi zote mbili kuwezesha kufanya utafiti semina mbali mbali na mafunzo ya muda mfupi na mrefu. 

 Ameeleza kwamba suala la Tafiti litaleta maendeleo ya taifa letu hivyo taasisi mbalimbali zisijikite katika ufundishaji tu bali ziende katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya kitanzania. Amesema kuwa matarajio yao ni makubwa sana katika kuongeza ufanisi na mashirikiano baina ya taasisi hizo mbili kuweza kutoa mafunzo yenye viwango yatakayosaidia katika ujenzi wa taifa letu. 

 Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa kijeshi Monduli {TMA} Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba amesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa katika kuwezesha Jeshi hilo kuendeshwa kiweledi. 

Amesema kwamba ni matarajio yao ni makubwa sana mojawapo ni kuongeza uwezo wao kitaaluma kwa kupitia tafiti mbalimbali na pia uwezo wa watu wao kutafuta majawabu ya changamoto za wananchi na jamii kwa ujumla. 

 Ameeleza kuwa suala la pili ni kupitia tafiti kuja na majawabu ya kuisaidia nchi yetu katika changamoto zinazoikabili nchi yetu katika Nyanja za kiuchumi kijamii na masuala mbalimbali yahusuyo nchi yetu kuweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo.


Share To:

Post A Comment: