Naibu Kamishna huduma za shirika , Needpeace Wambuya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo


Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Zaidi ya wananchi 5,000 wanaozunguka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wanatarajiwa kunufaika na mradi wa  chujio la kutibu maji unaotekelezwa na mamlaka hiyo katika eneo la( Mama HHau )wilayani Karatu mkoani Arusha.
Hayo yamesemwa leo   jijini Arusha na Naibu Kamishna huduma za shirika ,Needpeace Wambuya wakati akizungumza  na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo ambao unatarajiwa kuwanufaisha watalii wanaoingia katika hifadhi hiyo pamoja na wananchi kwa ujumla.
Amesema kuwa ,mradi wa teknolojia hiyo ya kisasa itaruhusu kiwango cha lita 1.5 milioni kutibiwa kwa siku  kiasi ambacho  kitatosheleza mahitaji ambapo hadi kukamilika unatarajiwa kutumia shs 859,000  milioni na kwa Sasa hivi umefikia asilimia 85 .

Amesema kuwa,maji yalikuwepo lakini kadri muda unavyozidi kwenda yamekuwa yakipungua ubora kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mazingira na wanyama ,hivyo ikawalazimu kuyatibu ili kufikia viwango vya kimataifa.

“mradi huu ulianza  Septemba mwaka Jana na unatarajiwa kukamilika june mwaka huu,na mbali na kuwanufaisha wananchi hao pia utaisaidia hospitali ya kilutheri Karatu  ambayo imekuwa ikiwahudumia wananchi mbalimbali “amesema .

Naye Meneja wa usimamizi wa mradi huo,Godlove Sengele   amesema kuwa ,kuwepo kwa mradi huo  kutamaliza tatizo la ubora wa maji katika maeneo ya  lango la Loduare,mahoteli ya kitalii,makao makuu ya NCAA, hospital ya kilutheri Karatu,pamoja na wananchi na hivyo kuweza kutoa huduma hiyo kwa viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.

“Mradi huu unajengwa ili kuboresha ubora wa maji yaliyokuwa yakitumiwa huku akiwataka  wananchi watarajie maji yenye ubora ambao unatambulika na WHO na TBS na kuweza kutambulika kimataifa.”amesema Sengele.
Nao baadhi ya wananchi ,Neema Mollel wakizungumza kuhusiana na mradi huo,wamepongeza kuwepo kwa mradi huo kwani utawasaidia  sana kuondokana na changamoto ya maji  ya uhakika ambayo hayachafuliwi na wanyama kutokana na kuchunjwa kabla ya kuwafikia wananchi.
Share To:

Post A Comment: