Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amezindua zoezi la upandaji miti katika Mtaa wa Mayombo Kata ya Iwambi Jijini Mbeya zoezi lililoratibiwa na Iwambi Active Group chini ya Mwenyekiti wake Melania Kifaru uzinduzi uliofanyika Shule ya Msingi Iwambi.


Akizindua zoezi hilo Mahundi amekipongeza kikundi hicho kwa kusema wanufaika wa zoezi hilo ni Wizara ya Maji ambao hutegemea miti kulinda uoto  wa asili na vyanzo vya maji.


"Naungana nanyi katika zoezi hili kama mkazi wa Iwambi pia kuungana na Mbunge wa Mbeya Dkt Tulia Ackson sambamba na Waziri ofisi ya Rais Mazingira Suleiman Jaffo",alisema Mahundi.


Awali Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Iwambi Elia Kasanga mbali ya kumshukuru Naibu Waziri wa Maji kushiriki zoezi hilo alimuomba computer kwa ajili ya matumizi ya shule ombi ambalo Naibu Waziri amekubali kulitekeleza mapema iwezekanavyo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Iwambi Active Group Melania Kifaru amesema jumla ya miti 2200 imepandwa katika taasisi za umma ikiwemo shule, zahanati na ofisi ya mtaa.


"Mbali ya miti kupandwa katika taasisi kila mwananchi amekabidhiwa miti mitatu ikiwemo ya matunda na vivuli kwa ajili ya kutunza mazingira",alisema Melania.


Zoezi hilo pia limehudhuriwa na Diwani wa Sinde Fanuel Kyanula kwa niaba ya Diwani wa Iwambi Humphrey Ngalawa ambaye amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki upandaji miti pia Naibu Waziri wa Maji kwa kukubali kushiriki ili Jiji la Mbeya liwe na mandhali nzuri na kulinda vyanzo vya maji.

Share To:

Post A Comment: