Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hassan Chande ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati akifungua kikao cha nne cha baraza kuu la nne la wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)   leo mkoani Singida.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango, Wakili Said Chiguma akizungumza kwenye baraza hilo.
Mwenyekiti wa baraza hilo, Dk.Momole Kasambala akitoa taarifa ya Taasisi hiyo mbele ya mgeni rasmi.
Makamu Mkuu wa Chuo, Fedha, Utawala na Mipango Dk. Isaya Hassanal akimshukuru mgeni rasmi baada ya kufungua baraza hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini Mhandisi Paskas Muragili akizungumza katika baraza hilo.
Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Daud Mashauri akizungumza kwenye baraza hilo.
Washiriki wa baraza hilo wakiimba wimbo wa mshikamano wa wafanyakazi.
Wimbo wa mshikamanoukiimbwa.
Taswira ya baraza hilo.
Muonekano wa baraza hilo.

Baraza hilo likiendelea.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Singida Mjini wakiwa kwenye baraza hilo.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Baraza likiendelea.

 Baraza likiendelea.



Na Dotto Mwaibale, Singida


TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeombwa kuangalia na kuchangamkia fursa kwa kufungua Tawi Zanzibar ili kutanua huduma zao na kufahamika kimataifa.

Ombi hilo limetolewaa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hassan Chande ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifungua kikao cha nne cha baraza kuu la nne la wafanyakazi wa TIA la siku mbili lililoanza leo mkoani Singida.

"TIA kufungua Tawi Zanzibar ni fursa kubwa kwani kunawanafunzi wanaosoma Chuo cha Fedha na Utawala Zanzibar (ZIFA) kutoka sehemu mbalimbali kama Malawi, Rwanda, Kenya, Ethiopia na Eritrea " alisema Chande.

Alisema ikitokea TIA wakafungua Tawi Zanzibar na kutokana na uzoefu wao wa muda mrefu wakiuona anaamini watajiunga na wakirudi kwao ni lazima wataenda kuitangaza taasisi hiyo hivyo ni muhimu TIA kufanya hivyo haraka iwezekanavyo badala ya kujifungia ndani.

Aidha Chande alisema TIA ilianzishwa kwa lengo la kutoa mafunzo, ushauri na kufanya tafiti kwenye maeneo ya Uhasibu, Ununuzi na Ugavi na maeneo mengine ya kibiashara.

Chande aliipongeza taasisi hiyo kwa kuendelea kutoa elimu yenye ubora ambayo ndio msingi mkuu wa mafanikio kwenye nchi yoyote inayotaka kuwa na maendeleo ambapo aliisisitiza taasisi hiyo kuongeza juhudi katika maeneo ya tafiti na huduma za ushauri ikiwa ni sehemu ya kuiwezesha kujitegemea kimapato na kuisaidia Serikali katika kutafuta suluhisho kwa changamoto mbalimbali zilizopo hususan katika tasnia ya Uhasibu na Fedha.

Alisema kupitia kikao hicho kama wajumbe wa baraza la wafanyakazi wanayo nafasi kubwa ya kuwaelimisha wafanyakazi wenzao kuhusu umuhimu wa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika sehemu yake ya kazi ili kufikia malengo waliojiwekea.

"Wakurugenzi Mameneja wa kampasi, Wakuu wa vitengo na idara wasimamie kwa dhati suala la maadili katika sehemu zao za kazi" alisema Chande.

Chande alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa dhati kuondoa uzembe na vitendo vyovyote vya rushwa mahali pa kazi hivyo basi ni wajibu wa kila mfanyakazi wa TIA kuhakikisha anafahamu wajibu wake mahali pa kazi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango, Wakili Said Chiguma akizungumza kwenye baraza hilo alitoa ushauri kwa TIA kuangalia uwezekano wa kutoa mafunzo kwa waadhiri na wakufunzi ambao nao watakuwa wakitoa ushauri nasaha kwa wanafunzi waliopo katika taasisi hiyo ili wajue wamalizapo masomo waondoe dhana ya kupata kazi nzuri na kuwa na maisha bora badala yake waone ni jambo la kawaida na kujipanga na maisha kwa kujiajiri na kuondokana na msongo wa mawazo wa kukosa kazi.

"Kumekuwa na matukio mengi ya vijana wanaomaliza masomo yao kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo baada ya kukosa kazi za kufanya hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuwaanda kisaikolojia kuwa baada ya kuhitimu masomo yao wasitegemee kuwa na maisha mazuri bali wajiandae kukiajiri" alisema Chiguma.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa baraza hilo , Dk.Momole Kasambala alisema baraza hilo kwa matakwa ya kisheria limewashirikisha viongozi wa TIA na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka kampasi sita za TIA ambazo ni Dar es Salaam, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Kigoma na wenyeji Singida.

Kasambala alisema Dira ya TIA ni kuwa Taasisi inayotoa elimu yenye ubora katika biashara, huduma za utafiti na ushauri barani Afika na kuwa kama taasisi ya elimu ya juu, majukumu yake makuu ni kutoa mafunzo, ushauri wa kitaalam na kufanya utafiti timizi kwenye nyanja bobezi.

Alisema TIA imeendelea kutimiza majukumu yake katika kuchangia maendeleo ya Taifa siyo tu kupitia mafunzo, bali pia katika kufanya tafiti na kutoa huduma ya ushauri kwenye nyanja bobezi hivyo kuchangia katika maendeleo ya viwanda na ukuaji wa uchumi wa nchi.

Aidha Kasambala alisema mafunzo yanayoendeshwa na Taasisi hiyo kwenye baadhi ya Halmashauri hapa nchini yamekuwa na mchango mkubwa katika ukusanyaji mapato na kubaini namna bora ya kudhibiti upotevu wa mapato kutokana na ukwepaji kodi na ushuru.

Makamu Mkuu wa Chuo, Fedha, Utawala na Mipango Dk. Isaya Hassanal akimshukuru mgeni rasmi baada ya kufungua baraza hilo alisema yale yote aliyoyaagiza watayatekeleza yakiwemo kutimiza wajibu wao sehemu za kazi, kufungua Tawi Zanzibar, kusimamia suala la maadili, kufanya kazi kwa bidii, kutekeleza malengo waliopangiwa katika muda waliopangiwa na maagizo mengine yote.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: