Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos, akizungumza na Madiwani katika mkutano wa kawaida wa robo ya pili wa Februari 23 na 24 wa mwaka wa fedha wa 2021/ 2022 uliofanyika jana wilayani humo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo James Mkwega.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo James Mkwega akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.

Madiwani wa Viti maalum wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Miriamu Hussein kutoka Kata ya Iguguno Tarafa ya Kinyagiri, Florence Misahi kutoka Nkinto Tarafa ya Kurumi, Habiba Omari kutoka Kinampundu Tarafa ya Nduguti, Maria Kitalama kutoka  Nduguti Tarafa ya Nduguti na Zaina Kihara kutoka Kinyagiri Tarafa ya Kinyagiri.
Kikao kikiendelea.

Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Kizigo  akitoa onyo kwa watu wanaojiita waganga wakienyeji maarufu kama lambalamba kuacha mara moja kupiga ramli chonganishi na kuwa atakayebainika akiendelea kufanya vitendo hivyo atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Katibu Tawala, Elizabeth Rwegasira, akichangia jambo kwenye kikao hicho..

Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.

 Katibu wa Vikao wa Halmashauru hiyo (CC), Daudi Makendi akiongoza kikao hicho.

Maswali yakiulizwa.
Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Kinampundu, Habiba Omary akiuliza swali. 
Duncan Kifaluka wa Idara ya Afya akijibu maswali kwenye kikao hicho. 
Diwani wa Viti Maalum wa Mkalama mjini, Zainabu Kihara akiuliza swali.
Afisa Elimu Taaluma Sekondari Ernest Stephene, akijibu maswali kwenye kikao hicho.
Maswali yakiulizwa.
Maswali yakiulizwa.
Taswira ya kikao hicho.
Afisa Utamaduni Nicodemo Kagete akijibu maswali.
Wakuu wa Idara na wataalam wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Francis Isack, akichangia jambo kwenye kikao hicho. 
Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) wilayani humo, Mhandisi Mang'ara Magoti, akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara katika halmashauri hiyo.
 


Na Dotto Mwaibale, Mkalama Singida


MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida wamezuia tabia ya uhamisho wa walimu wa shule za msingi wilayani humo baada ya kuwepo kwa hamisha hamisha ya walimu wakuu wanaolalamikiwa na kuzua malalamiko.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo James Mkwega alitoa zuio hilo baada ya madiwani kuadhimia kwa pamoja kusitisha uhamisho huo katika mkutano wa kawaida wa robo ya pili wa Februari 23 na 24 wa mwaka wa fedha wa 2021/ 2022 uliofanyika jana wilayani humo. 

"Nina agiza kuanzia sasa uhamisho wa walimu wakuu wanaolalamikiwa katika halmashauri yetu usitishwe mara moja kwani malalamiko yamekithiri na tunayajua mengi yanayosababisha kuwepo kwa uhamisho huo" alisema Mkwega.

Mkwega aliwaomba viongozi wa sekta ya elimu wilayani humo kuzingatia jambo hilo kwa maslahi mapana ya kuinua taalamu kwa wanafunzi na si kubebana ambapo aliwaomba viongozi hao kutowafumbia macho walimu wanaoboronga na kuwataka waondolewe na ikiwezekana wawaingize vijana wenye sifa badala ya kuwang'ang'ania wazee.

Katika hatua nyingine Mkwega alipiga marufuku tabia ya wakuu wa idara kutoa vipuri vya magari ya halmashauri hiyo yenye changamoto ndogo na kuhamishia kwenye magari mengine ambapo alisema jambo hilo haliwezekani na atakaye bainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Akitolea mfano wa gari moja lililokuwa na matairi ambayo yalichukuliwa na kwenda kufungwa kwenye gari lingine na kuliacha gari hilo lililokuwa na changamoto ndogo likiendelea kuharibika na sasa lipo kwenye hatua ya kupigwa mnada.

Mkwega alitumia baraza hilo kuwaomba madiwani hao kwenda kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi na mpango wa anuani za makazi na kutunza mazingira yasiharibiwe kwa kuchimba mashimo karibu na barabara wakati wa uchimbaji wa madini kwani miundombinu hiyo imekuwa ikijengwa kwa fedha nyingi na Serikali.

Wakichangia kuhusu changamoto ya kuwahamisha kiholela walimu hao baadhi ya madiwani walionesha kukerwa hasa baada ya kuibuka kwa kasi ya hamisha hamisha hiyo ya walimu wakuu wa shule mbalimbali ambapo walidai viongozi wa sekta ya elimu wamekuwa na maslahi na baadhi ya walimu hao.

"Baadhi ya walimu ambao wamekuwa wakihamishwa kwenda shule B wamekuwa wakituhumiwa kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ubadhilifu wa fedha lakini viongozi hao baada ya kushughulikia tuhuma hizo wamekuwa wakiwahamisha na kwenda kushika nafasi hiyo hiyo katika shule nyingine" alisema mmoja wa madiwani hao.

Alisema katika shule zingine ambazo zilikuwa hazina maendeleo kuna baadhi ya walimu waliozipambania kwa kuziboresha kuanzia ufaulu, mazingira na kuwaweka pamoja kati ya walimu, wanafunzi na wananchi lakini viongozi hao wa elimu wamekuwa wakiwaondoa na kuwahamishia kwenye shule zingine duni na wale wenye tuhuma mbalimbali wakihamishiwa kwenye shule hizo jambo ambalo limeonesha kuwagawa walimu hao na kuwachukia viongozi wao huku viwango vya taaluma vikiporomoka.

Baadhi ya mambo mengine yaliyojiri kwenye baraza hilo ni maswali ya papo kwa papo ambapo Diwani Amri Juma kutoka Kata ya Msingi aliuliza swali  kutaka kujua ni lini wilaya hiyo itapata mahakama ya baraza la nyumba na ardhi na kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma hiyo Kiomboi Iramba.

Swali lingine lililoulizwa ni la kutoka kwa Diwani wa Viti Maalum Zainabu Kihara ambaye alitaka kujua ni wanafunzi wangapi walioacha shule kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ya kupata mimba ambao wamerudi shule kama Serikali ilivyotangaza mpango huo ambapo alijibiwa na Afisa Elimu Taaluma Sekondari Ernest Stephene kuwa ni wanane na kuwa kila mmoja alirudi kwa hiyari na sasa wanaendelea na masomo katika shule walizokuwa wakisoma awali.

Maswali mengine yaliulizwa na Diwani Barnaba Mang'ola wa Kata ya Iguguno, Florence Misahi kutoka Nkinto na kupatiwa majibu na wakuu wa idara na wataalamu wa wilaya hiyo.

Majibu mengine yalitolewa kiufasaha na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Asia Messos kwa kushirikiana na wataalamu kutoka idara mbalimbali.

Messos alisema halmshauri hiyo imejipanga kujenga hosteli katika shule za sekondari ili kuwapunguzia wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni na kurudi nyumbani jambo litakalosaidia kuongeza ufaulu.

Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Kizigo ambaye alikuwepo kwenye baraza hilo alitumia nafasi hiyo kuwaonya watu wanao jiita ni waganga wa kienyeji maarufu kama lambalamba ambao wanaingia wilayani humo na kupiga ramli chonganishi na kuwashika watu uchawi kuwa waache tabia hiyo mara moja kwani Serikali haiwezi kuwavumilia.

Alisema awali baada ya kukamatwa kwa watu hao masuala ya kisiasa yaliingia kwa baadhi ya viongozi kumpigia simu wakiomba waachiliwe na kuwa sasa wakikamatwa kwa kufanya hivyo wasithubutu kumpigia simu kwani lambalamba hao wanahatarisha maisha ya watu wanao wataja na kuwa wanachofanya ni kuvunja haki za bnadamu.anzia leo watu wote wanaoshirikiana na lamba lamba hao iwe kwa kuwaleta, kukusanya fedha za kuwalipa au kwa namna yoyote ile tutawakamata na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria" alisema Kizigo.

Baadhi ya viongozi waliopata fursa ya kuchangia mambo mbalimbali kwenye baraza hilo ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Kaskazini, Francis Isack, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Lameck Itungi, Katibu wa CCM wilaya, Martha Zingula, Afisa Uchaguzi, Abdallah Njelu, Katibu Tawala, Elizabeth Rwegasira, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Samuel Bosco, Katibu wa Vikao wa Wilaya hiyo (CC) Daudi Makendi na Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) wilayani humo, Mhandisi Mang'ara Magoti.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: