Habari za muda huu rafiki yangu, bila shaka u mzima na unaendelea na utaraitibu wako wa kila siku wa kutafuta griss ili kulaini vile vyuma vilivyokaza.

Na siku ya leo naomba tujifunze kwa pamoja kuhusu ni kwa namna gani tunaweza kuachana na michepuko, kwani nimekuwa nikipokea jumbe nyingi sana za wasomaji wangu,  wengi wakiniuliza afisa mipango nifanye nini ili niweze kuachana na mchepuka na kubaki njia kuu?

Nami bila hiana naomba nitirike hapa siku ya leo ili niwaponye wengi kwani swali la aina hii limekuwa likiwatesa wengi,  kwa sababu wengi wa wanaume au wanawake ambao wanachepuka imekuwa ni suala gumu sana kuweza kuondoka katika mchepuko na kubaki njia kuu.

Mtego ambao umekuwa unatumiwa na michepuko kuwanasa wapenzi wa watu wengine, umekuwa upo vizuri kwa sababu pindi watu wanasapo imekuwa ni ngumu sana kunasuka. Kama na wewe ni miongoni mwa watu hao ambao wamekuwa wakichepuka na wameshindwa kunasuka unachotakiwa kufanya ni;

1. Unapokuwa upo pamoja na mchepuko au wahenga wa hivi karibuni huita hawala, unachotakiwa kufanya ni kumsimulia mchepuko wako mambo mengi mazuri ambayo huwa unafanya uwapo na njia kuu. Kama hiyo haitoshi msimulie mchepuko  kuhusu uzuri wa njia kuu pasipo kuona aibu wala kukosoa uzuri na ubaya wa njia kuu. Kufanya hivyo itamsaidia mchepuko huyo ajisikie vibaya kwani michepuko mingi huwa haipendi kusikia habari zinazohusu njia kuu.

2. Punguza mawasiliano na Mchepuko.
Nafahamu fika wakati unapoanza mahusiano na huyo ambaye unamuita after baby mawasilino yalikua ni mazuri sana. Vivyo hivyo kama unataka kuachana na mchepuko  wako basi unatakiwa kufanya ni kufanya kinyume chake, yaani mawasilino yawe ni finyu ikiwezekana yafe kabisa. Muda mwingine akikupigia simu ona kama umeona moto unaowaka.

Mpaka kufikia hapo si la ziada mwisho nimalize kwa kusema  " Mchepuko ni dili feki, tafadhari baki njia kuu.
Share To:

Post A Comment: