Uploading: 12887439 of 12887439 bytes uploaded.


 DIWANI wa Kata ya Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Salome Nelson Mnyawi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea darasa jipya lililomaliza changamoto ya mrundikano kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari Tanzanite.


Salome akizungumza alisema darasa hilo limemaliza tatizo la wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza wa shule hiyo kukosa nafasi kwenye wakati wa kusoma kwenye shule hiyo.

Amesema serikali ya awamu ya sita ilitoa sh20 milioni kupitia fedha za miradi ya maendeleo ya Uviko-19 na kujenga darasa na madawati ya wanafunzi.

"Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan kwani wanafunzi wote wa kidato cha kwanza wamepata nafasi na wameingia kusoma kwenye shule hii," amesema Salome.

Hata hivyo, ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kwa kutoa sh32 milioni za miundombinu ya shule hiyo ya sekondari Tanzanite.

"Kupitia fedha hizo tulizopatiwa na halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, tumeweza kujenga darasa jipya, ofisi ya walimu na kukamilisha vyumba sita ya vyoo vya wanafunzi," amesema Salome.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani, Adam Kobelo amesema changamoto ya barabara ya shule hiyo inafanyiwa utatuzi.

Kobelo amesema wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) wa wilaya ya Simanjiro, unakagua na kujipanga namna ya kutengeneza barabara ya kufika kwa urahisi hapa shuleni.

Mkuu wa shule ya sekondari Tanzanite, Jude Mziray amewaasa wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wanapeleka chakula shuleni hapo ili wanafunzi wale.

"Huwezi kuwafundisha wanafunzi wakiwa na njaa na wakaelewa hivyo suluhisho ni chakula shuleni, wazazi na walezi wajitahidi kwenye hilo kwani ni wajibu wao," amesema Mziray.
Share To:

Post A Comment: