Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Comrade Baraka Ramadhani Shemahonge 
***

Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga wamewaonya viongozi wa chama hicho na serikali wanaoleta lugha za kejeli na kubeza jitihada za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhu wakimtaka Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ajitathmini na kujitafakari yeye pamoja na genge lake kama wanastahili kuendelea kuwemo kwenye vyombo vya maamuzi katika Taifa.

Hii hapa ni taarifa iliyotolewa na UVCCM Mkoa wa Shinyanga leo Januari 5,2022.

🟢 UVCCM MKOA WA SHINYANGA YAWAONYA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI WANAOJARIBU  KUMKWAMISHA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN💪🏻🙏

Imetuchukua muda usiozidi nusu saa tu kuelimisha Taifa nini faida za nchi kukopa kama faida.

Taasisi za kimataifa za fedha  kama
💵IMF 💵WB 💵ADB nk zisingekuwepo kama umuhimu wa mataifa kukopa usingekuwepo.

Rais Mama Samia Suluhu Hassan si wa kwanza kukopa, watangulizi wake wote walikopa na hata hao wanaopinga mikopo leo ikitokea genge lao lime bahatika kupewa nchi, watakopa tu.

Sisi Vijana wa Mkoa wa Shinyanga tumefanya ziara ya kukagua miradi iliyogharimu Sh. bilioni 17 katika mkoa wetu  wa Shinyanga kutoka kwenye serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan

👉Bilioni 9 ni kwa ajili ya madarasa ya shule za sekondari na shule za msingi

👉Shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya vituo vya afya

👉Shilingi Bilioni 6 kwa ajili ya hospitali yetu ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga

Sisi vijana wa CCM Mkoa wa Shinyanga tunasimama na Mama  yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo anayouletea mkoa wa Shinyanga na  Taifa letu kwa ujumla. 

Tunaendelea kuwaonya wote wanaoleta lugha za kejeli na kubeza jitihada za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na hao wanaotumwa na mabwenyenye au  kwa maslahi yao binafsi, tunaahidi tunapambana nao usiku na mchana kwa maslahi mapana ya maendeleo ya Taifa letu

Vijana wa CCM Mkoa wa Shinyanga tunamtaka Mhe. Job Ndugai ajitathmini na kujitafakari yeye pamoja na genge lake kama wanastahili kuendelea kuwemo kwenye vyombo vya maamuzi katika Taifa letu


January 5, 2022 
Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Comrade Baraka Ramadhani Shemahonge 💪🏻
Share To:

Post A Comment: