Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolfu Mkenda amesema serikali itaanzisha mkakati wa kufanya tathmini ya kufuatilia wahitimu ya vyuo vya ufundi nchini ili kufahamu taarifa zao na kuweza kupata mrejesho wa kile walichokipata vyuoni.

Akizungumza katika hafla ya kutunuku vyeti kwa wanagenzi wahitimu wa mpango wa urasmishaji ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi,Prof,Mkenda alisema njia hiyo itasaidia serikali kupata mrejesho wa wahitimu walipofikia katika nafasi za ajira hali ambayo itawasaidia kujihimarisha.

Prof.Mkenda alisema wangependa wale wanaoanzisha hoteli  wawaajiri watu wenye vyeti vya veta kwani wanahitaji katika ujenzi unaoendelea wachukuliwe watu wenye sifa ili serikali iweze kujivunia kutokana na huduma zinazotolewa na wahitimu kutoka vyuo vya ufundi nchini.

"Na kama umejiajiri na unatoa huduma bora inayotambulika na watu kupitia ujuzi aliyoupata katika vyuo vya ufundi Veta lazima mabadikio yatatokea katika jamii inayokuzunguka,"alisema Prof.Adolfu Mkenda.


Mkenda alisema"Wako wagenzi ambao ni mafundi magari walikuwa wanatengeneza pasipo kuwa katika mfumo rasmi lakini sasa wamerasmisha ujuzi wao hali ambayo itakwenda kurasmi lengo ni kukuza ujuzi kwa vijana na pia isijetokea ajira wakapatikana watu wa kusema kuwa elimu yetu haina wanaoajirika."

Aidha aliongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni uhitaji wa wanafunzi kusoma kwa bidii na kujituma kwasababu elimu aina mwisho na wanaohitimu leo asipatikane wakuwadanganya bali jiendelezeni  zaidi ili huduma ziweze kutambulika.

"lakini kwa upande wetu sisi tumewasimamia utoaji wa mafunzo haya na tutafatilia wanafunzi wetu baada ya kuhitimu wanaenda wapi,wanafanya kazi maeneo gani au wamejiajiri wapi pamoja kujaribu kuwauliza waajiri juu ya utendaji kazi wao sababu ndani ya Chama chamapinduzi wanataka ajira milioni nane ifikapo 2025,"alisema Prof.Mkenda.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa nchi,ofisi ya waziri mkuu kazi,ajira na watu wenye ulemavu,Patrobas Katambi alisema kuna baadhi ya halmashauri kuna vikundi hewa hivyo wana haja ya kujiridhisha ili kuondoa urasimu huo.

"Katika Taifa letu nchini Tanzania nafasi kubwa tangu kuanza kwa awamu hii ya sita uwakilishi wa vijana umekuwa mkubwa sana hivyo ni jukumu la vijana kumuunga mkoa Rais Samia Suluhu Hassani,"alisema Naibu waziri Katambi.

"Kinachohitajika sisi kama wajibu wa serikali kwa mujibu wa ibara ya 11 kutengeneza mazingira wezeshi yanayotolewa na ofisi ya waziri mkuu lakini pia ofisi ya Rais Tamisemi na ndio maana kuna mikopo ambayo halmashauri zote nchini zinatoa,"alisema Katambi.

Katambi alisema kumbe elimu pekee sio ngao ya kumkinga mtu na umasikini bali ni nyenzo wezeshi ya kumsaidia mtu kupambana na umasikini.

"Tunahitaji maarifa na vijana wa Taifa hili tuwabadilishe kwanza mtazamo kwani kumekuwepo na malalamiko sana kwa vijana juu ya kazi na ajira lakini sababu zinazochangia ni kutotumia vizuri fursa zinazotolewa na serikali wakati mwingine  vijana wamekuwa na uvivu wa kuchagua kazi pamoja na changamoto ya kutokujua mahali pakusaidiwa,"alisema Naibu waziri wa kazi ajira na watu wenye ulemavu.

Alisema kazi kubwa ambayo wanayo kama serikali,upande wa jamii pamoja na mamlaka zote ni kuwasaidia vijana kuwa na mitazamo chanya dhidi ya Taifa lao lakini pia kuwa na uzalendo.

Share To:

Post A Comment: