Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima akikagua miundombinu ya barabara  wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja aliyoifanya leo ya kutembelea miradi hiyo na kuona maeneo korofi ili yatafutiwe ufumbuzi.
Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima akikagua miundombinu ya barabara.
Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi alioambatano nao kwenye ziara hiyo. Kulia ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Shabani Hamisi.
Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Mnung'una wakati wa ziara hiyo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


MBUNGE wa Singida Mjini Mussa Sima amefanya ziara  ya kutembelea miundombinu ya barabara na maeneo korofi ili yatafutiwe ufumbuzi.

Akizungumza katika ziara hiyo aliyoifanya leo alisema anataka kuona maeneo yote korofi katika barabara zote ziliopo jimboni humo yanatafutiwa ufumbuzi kwa kuyamaliza haraka iwezekanavyo.

"Hakuna sababu ya kuwa na maeneo korofi kwenye barabara zetu wakati Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan ametupa Sh. 2.2 Bilioni kwa ajili ya kujenga miundombinu ya barabara nachukua nafasi hii  kumpongeza kwa niaba ya wananchi wa jimbo letu" alisema Sima.

Maeneo aliyoyatembelea ni barabara inayotengenezwa Mwamise na Unyankhae Kata ya Mandewa pamoja na kuangalia maeneo korofi yanayohitaji kufanyiwa kazi yaliyopo Mtaa wa Mnung’una Kata ya Minga.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: