Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Mhe Raymond Mwangwala amezitaka taasisi, Mashirika na Wananchi kupanda miti kwa wingi hususani kipindi hiki cha mvua kwani miti inamanufaa makubwa kimqzingira.
Mwangwala amesema hayo wakati akikagua kitalu cha miti zadi ya 600,00 kinachosimamiwa na Wakala huduma za Misitu Tanzania ( TFS).
" Ukataji miti hovyo maeneo ya Loliondo haukubaliki ,niwatake Wananchi kufuata utaratibu wa kukata miti tunataka mti mmoja ukikaywa ipandwe miti hata 20"amesema"
Naye Mhifadhi Misitu Wilaya wa Ngorongoro (TFS) Bw.Major Ngoilenya amesema TFS imerahisisha upatikanaji wa Miti ambapo miti yote inayozalishwa katika kitalu hicho inatolewa kwa wananchi bila malipo." Niwakaribishe Wananchi kuja kupata mitii tutunze mazingira yetu" amesema.
Post A Comment: