Serikali imesema itaendelea kutoa kipaumbele katika kuwekeza kwenye Sekta ya Elimu kwa kuendelea kuongeza bajeti katika sekta hiyo mwaka hadi mwaka kutoka asilimia 18.7 ya bajeti Serikali ya mwaka 2021/22 hadi  kufikia asilimia 20 ifikapo mwaka 2025 ili kuwezesha utoaji wa elimu bora kwa wote.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza katika kilele cha Mkutano wa Elimu wa WirED Jijini Dubai ulioshirikisha wadau kutoka Nchi mbalimbali duniani ambao wamejadili kuhusu uwekezaji katika Elimu pamoja na uimarishaji wa masuala ya Sayansi na Teknolojia katika karne ya 21.


Ndalichako amesema kuendelea kuongezeka kwa uwekezaji huo kunatokana na utashi wa kisiasa ambao pia umewezesha serikali kuwa mifumo thabiti ya usimamizi wa rasilimali za elimu.


 Ameongeza  kuwa Serikali inatambua  na kushukuru mchango mkubwa wa wadau wa maendeleo na sekta binafsi katika sekta ya Elimu. 


Mkutano huo umehudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambae ni  Mwenyekiti Mfuko wa Washirika Wafadhili wa Sekta ya Elimu Duniani, _Global Partnetship in Education (GPE) na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambae pia amezungumzia utayari wa Serikali katika kuongeza uwekezaji katika Elimu.

Share To:

Post A Comment: