Mbunge wa viti maalum Vijana (CCM) Asia Halamga ameweka wazi kwamba hana mpango wa kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo ifikapo 2025 kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakimuhisi, akisema kuwa kwa sasa ni Mbunge ndani ya Miaka mitano bado hajajua kesho yake,Mungu ndo anajua.

Mbunge wa vijana Asia Halamga amesema hana mpango wa kugombea ubunge kama inavyozungumzwa na baadhi ya watu Kwani nafasi aliyonayo inamtosha; “Sijawahi kuzungumza popote kuhusu kugombea jimbo la Hanang.

Mimi ni Mbunge wa Vijana Taifa, Hanang ni kwetu lazima nitoe msaada pale inapobidi, watu wasinifanye niogope kutoa michango mbalimbali.Alisema Asia
"Kwa sasa mimi ni Mbunge ndani ya Miaka mitano, ndo kwanza mwaka wa kwanza wala sijui kesho yangu,sijafikiria kugombea jimbo lolote" alisisitiza Mbunge huyo.

Share To:

Post A Comment: