Paroko wa  Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Simion Gwanoga (kulia)  na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania for Equal Opportunity (TAFEO) na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya chakula cha Krismasi kwa watu wa makundi maalumu, Stella Mwagowa (katikati) na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Moses Msai wakikata keki maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe hiyo iliyofanyika  Ukumbi wa Social mjini hapa jana. Katikati ni mtoto kutoka kundi maalumu aliyewawakilisha wenzake katika tukio hilo la kukata keki.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Victorina Ludovick ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania for Equal Opportunity (TAFEO) na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya chakula cha Krismasi kwa watu wa makundi maalumu, Stella Mwagowa, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Hamasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Singida mjini, Yahaya Njiku akionesha upendo kwa kumlisha chakula Idrisa Abdallah mkazi wa Utemini mjini hapa wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Vinywaji na Mratibu wa Taasisi ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida  Shabani Munkee akiwapa chakula vijana kutoka kundi maalumu wakati wa hafla hiyo.
Watoto kutoka kundi maalumu wakiimba wimbo wa Taifa kwa kuonesha ishara ya vidole.

Katibu wa Jumuiya hiyo na kamati ya maandalizi Edmund Mwambashi akiwajibika wakati wa hafla hiyo


Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

Paroko wa  Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu,  Simion Gwanoga akishiriki furaha na wazee waliofika kwenye hafla hiyo.
Sherehe ikiendelea. kutoka kushoto ni mdau wa maendeleo Mzee Honest Mushi, Dada Baptista Mameho kutoka Caritas Singida na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania for Equal Opportunity (TAFEO) Stella Mwagowa,
Sherehe ikiendelea.
Chakula kikichukuliwa tayari kwa kuliwa.


Chakula kikiliwa.
Hafla ikiendelea.
Watoto kutoka makundi maalumu wakishindana kula matikitimaji wakiwa wamelala baada ya kushiriki chakula kilichoandaliwa na Shirika hilo.

Wakati wa kula keki ukiendelea.
Picha ya pamoja baada ya hafla hiyo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


SHIRIKA la Tanzania for Equal Opportunity (TAFEO) lenye makao yake makuu mkoani Singida linalojihusisha na kutengeneza urafiki na watu wanaoishi mazingira magumu wakiwepo Yatima kupitia Jumuiya ya Sant Egidio limewakutanisha watu kutoka makundi maalumu zaidi 700 ndani ya Manispaa ya Singida kwa ajili ya kupata mlo wa pamoja  kusherehekea Sikukuu ya Krismasi.

Akizungumza jana wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Social mjini hapa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo, Stella Mwagowa alisema shirika hilo linafanya kazi zake kwa kushirikiana na jumuiya yake ya vijana wa vyuo wanao jitolea kupitia Sant Egidio.

Alisema watu wanaowalenga kufanyanao urafiki ni Yatima, wajane, watu wenye ulemavu na watoto waishio katika mazingira magumu.

Alisema katika hafla hiyo ambayo huifanya kila mwaka waliwaalika wageni mbalimbali ili kushuhudia na kujua namna ya kuyahudumia makundi haya ambapo pia wapo watu wenye ulemavu, watu wasio na afya, wenye changamoto ya akili, na wasio sikia.

Mwagowa alisema jumuiya hiyo ilianza mwaka 2011 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro baada ya yeye na baadhi ya watu wachache wakiwa chuoni hapo kuanza kufanya huduma za kuwatembelea wahitaji na kujenga urafiki nao na kuwatafutia misaada hivyo mwaka 2011 waliweza  kuungana na jumuiya  ya Sant Egidio  ambayo chimbuko lake ni Roma Italy baada ya kuona wanachokifanya kinafanana  hivyo wakaona nao waianzishe hapa nchini kwa kuanzia Mkoa wa Morogoro. 

"Egidio ni jina la mtu anayeishi huduma hii tunayoifanya wakatoliki tunaita Mtakatifu na kwa kuwa jumuiya hii ilianza  na vijana wakatoliki ndio maana tukaamua  tulienzi jina lake" alisema Mwagowa.

Alisema tangu mwaka 2011 walipoianzisha jumuiya hiyo sehemu mbalimbalo hapa nchini wamekuwa wakifanya kazi za kujitolea bila ya kupata ufadhili wowote.

Alisema kwa Singida walianza rasmi mwaka 2016  kwa kuwashirikisha vijana wa Chuo cha  Uhasibu, Utumishi na vijana wanaopenda kazi za jamii.

Alisema  jumuiya hiyo ina vijana wapatao 80 wengi wakiwa ni wanachuo na kuwa haibagui dini wala jinsia na kuwa wamefanikiwa kujenga urafiki na wakimbizi wa Mkoa wa Kigoma kutoka kambi za Mtendeli na Nyarugusu baada kuwatembelea ambapo mmoja wa wakimbizi hao naye kupenda kuanzisha jumuiya hiyo na wamejenga mahusiano makubwa. 

Alisema akiwa mmoja wa waanzilishi wa jumuiya hiyo walianza na vijana 10 lakini sasa wapo vijana wapatao 10,000 katika mikoa mbalimbali kupitia wana vyuo wanaomaliza masomo yao kusambaa hivyo kuwa fursa nzuri ya kujulikana.

Mwagowa aliwataja baadhi ya wadau waliofanikisha hafla hiyo kuwa ni CaritasA Katoliki, Baba Askofu Edward Mapunda, Mganga mkuu wa mkoa ,  Mkuu wa Mkoa Mtaafu wa Singida Dkt. Rehema  Nchimbi, Vijana wa Sisi Tanzania, Vijana wa Magufuli,  (African Geneus), Madiwani wa Kata ya Kinyeto na Mandewa, Bonite,Kijiji cha Nyuki,wafanyabiashara, wadau wa masuala ya kijamii na waandishi wa habari.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Victorina Ludovick ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo aliwashukuru waandaaji wa hafla hiyo na kuwa hafla za namna hiyo zimekuwa zikijenga upendo baina yao.

Ludovick alitumia nafasi hiyo kuhamasisha kupata chanjo ya Uviko 19 kwa watu wote na kuwa chanjo hiyo ni salama.

Paroko wa  Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu,  Simion Gwanoga ambayo hafla hiyo ilifanyika katika eneo lake alisema hafla ya mwakani itakuwa nzuri zaidi kwani wataanza maandalizi mapema tofauti na mwaka huu.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: