Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) leo Desemba 17,2021 ametembelea banda la Tanzania, Oman na Thailand kwenye Maonesho ya Dunia ya Expo 2020 Dubai yanayoendelea Dubai.


Katika ziara hiyo, Mhe. Prof. Kitila mkumbo aliongozana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb), Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Mtonga na Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi, Balozi Edwin Rutageruka.


Akiwa katika banda la Tanzania Prof. Mkumbo alizungumza na washiriki kutoka nchini Tanzania kuangalia namna ya kuboresha banda hilo pamoja na kuweka mikakati ya kuvutia wawekezaji nchini Tanzania.


Aidha, Prof. Kitila Mkumbo amewataka washiriki hao kujiandaa vyema kwa ajili ya “ _Tanzania Day_ ” itakayofanyika 26 Februari 2021 yenye lengo la kuitangaza Tanzania katika uwekezaji, utalii na biashara.


Katika mabanda ya Oman na Thailand Mhe. Kitila Mkombo alijionea namna ambavyo teknolojia imetumika katika kuonesha mafanikio na uwekezaji uliopo katika nchi hizo.

Aidha Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa kwanza wa Biashara wa (B2B) utakofanyika kesho tarehe 18 Desemba, 2021.Share To:

Post A Comment: