Na Rhoda Simba,Dodoma.

WAZIRI wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkesha wa mwaka mpya  kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,mkesha wa kuliombea taifa pamoja na viongozi mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo  Disemba 29 jijini hapa, na Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Fellowship of Churches Dk Godfrey Malassy  na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkesha mkubwa wa mwaka mpya ambapo amesema kuwa mkesha huo unalenga kuliombea taifa.

Amesema katika mkesha huo ambao utafanyika katika uwanja wa Jamhuri kuamkia mwaka mpya wa 2022 Rais amemtuma Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi kuwa mgeni rasimi kwa niaba yake.

Dk Mallasy amesema kuwa nchi ya Tanzania inatakiwa kuendelea kuwa na amani,upendo na ushirikiano wa kweli.

Aidha amesema kuwa, mkesha huo utahakikisha unafanya maombi kwa ajili ya kuliombea taifa kutoingia katika machafuko pamoja na watumishi wa umma.

"Tumekuwa tukishuhudia machafuko yakitokea katika  mataifa mbalimbali na machafuko  haya yanasababishwa na  kukosekana kwa amani na kudhoofika kwa uchumi,

"Watanzania tunatakiwa kulinda sana amani na kuhakikisha upendo unaendelea kati ya mtu na mtu pamoja na jamii kwa ujumla wake"amesema Mallasy.

Mwisho.

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Share To:

RHODA SIMBA

Post A Comment: