Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini na Katibu wa CCM Kata ya Mandewa Yusuph Kijanga Makera akihutubia mahafali ya 13 ya Shule ya Sekondari Mandewa iliyopo Manispaa ya Singida kwa niaba ya mbunge jana.

Baadhi ya wageni mashuhuri waliohudhuria mahafali hayo wakiongozwa na Yusuph Makera Kijanga (wa tatu kulia) wakijiandaa kukata keki ya mahafali, zoezi lililokwenda sambamba na harambee fupi iliyolenga kukusanya kiasi cha fedha kwa ajili ya kufanikisha mahafali hayo.
Wahitimu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye sherehe hizo.
Wahitimu wakiimba wimbo maalumu. 

Wazazi wa wahitimu na wananchi wengine wakifuatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Ramadhan Sima iliyosomwa na mwakilishi wake ‘Kijanga.’

Baadhi ya wageni walioketi meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye sherehe hizo.
Wazazi na wahitimu wakifurahi. 
Sherehe zikiendelea.
Sherehe zikiendelea.
Baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari Mandewa wakiwa kwenye sherehe hizo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mandewa, Georgia Maghiya akicheza na kufurahi wakati wa mahafali hayo.

Wahitimu wakifuatilia burudani mbalimbali kwenye mahafali hayo.
Mwonekano wa miradi ya majengo mbalimbali ya vyumba vya madarasa ambayo baadhi imekamilika na mingine kuwa katika hatua za mwisho za kupaua ambayo fedha yake ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Mwonekano wa miradi ya majengo mbalimbali ya vyumba vya madarasa ambayo baadhi imekamilika na mingine kuwa katika hatua za mwisho za kupaua ambayo fedha yake ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Mwonekano wa miradi ya majengo mbalimbali ya vyumba vya madarasa ambayo baadhi imekamilika na mingine kuwa katika hatua za mwisho za kupaua ambayo fedha yake ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Mwonekano wa miradi ya majengo mbalimbali ya vyumba vya madarasa ambayo baadhi imekamilika na mingine kuwa katika hatua za mwisho za kupaua ambayo fedha yake ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.


Na Godwin Myovela, Singida


MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameishukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa msukumo wa kipekee katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu mbalimbali ya elimu inayolenga kuinua tija na ustawi kwa ukuaji wa sekta ya elimu ndani ya jimbo lake.

Aidha, Mbunge huyo pamoja na mambo mengine, amekabidhi vifaa vya Tehama kwa shule ya Sekondari Mandewa ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zake za kuinua taaluma na viwango vya ufaulu ndani ya shule zote zilizopo ndani ya Jimbo la Singida Mjini kwa minajiri ya kuchagiza kasi ya ufaulu na uwajibikaji.

Akizungumza kwenye Mahafali ya 13 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Mandewa iliyopo ndani ya Manispaa ya Singida mkoani hapa jana, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mandewa Yusuph Kijanga Makera kwa niaba ya Mbunge huyo alisema muda mfupi ujao miradi hiyo inakwenda kupanua wigo wa fursa kwa watoto na vijana kujipatia elimu stahiki kwenye nyanja za mazingira rafiki.

“Tunaendelea kumshukuru Rais na chama chetu kwa mapenzi makubwa kwa wananchi wa mkoa wa Singida katika jitihada za wazi za utekelezaji wa maelekezo ya Ilani ya CCM kwa vitendo. Mpaka sasa zaidi ya majengo ya miundombinu mbalimbali ya kujifunzia takribani 42 ndani ya jimbo hili yapo kwenye hatua za mwisho za kukamilika,” alisema Makera kwa niaba ya Mbunge.

Akihutubia mamia ya wazazi na wananchi waliohudhuria mahafali hayo Makera alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha hatua kwa hatua inakwenda kupunguza changamoto nyingine zote zilizosalia kwenye sekta ya elimu, afya, maji, nishati, kilimo na nyinginezo, ili kujenga ustawi na tija kwa uwiano wa matokeo chanya katika muktadha wa kuinua kipato kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa.

Kwa niaba ya Mbunge Sima, aliwasihi wakazi wa Singida Mjini, hususan wazazi wanaozunguka Kata ya Mandewa kuendelea kuchapa kazi, kuwa wazalendo, kumuunga mkono Rais Samia kwa majukumu mazito aliyoanza nayo kwa kasi na mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi, na zaidi kukiamini Chama Cha Mapinduzi ambacho ndio taswira na mwelekeo katika mageuzi yaliyopo ya kiuchumi.

Aidha, Makera aliwataka wahitimu wapatao 163 wa shule hiyo kujikita katika kudumisha nidhamu, maadili, uzalendo na kuwaheshimu wazazi katika kipindi hiki wanapokuwa nje ya mikono ya walimu wao kama nyenzo ya kuwawezesha kuvuka salama dhidi ya vishawishi na makundi maovu ya mitaani vinavyoweza kuhatarisha maono ya ndoto zao katika kufikia mafanikio.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo Georgia Maghiya, alisema mpaka sasa tayari serikali imewakabidhi kwa nyakati tofauti jumla ya shilingi milioni 173-fedha za EP4R na Uviko 19 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na  matundu ya choo na baadhi ya miradi hiyo ipo mbioni kukamilika huku mingine ikiwa tayari imeanza kutoa huduma kwa walengwa.

Hata hivyo pamoja na kushukuru serikali na Mbunge kwa jitihada zinazoelekezwa kwa shule hiyo-ikiwemo ugawaji wa vifaa hivyo vya Tehama, Maghiya alimuomba Mbunge kuangalia uwezekano wa kumaliza changamoto ya ukosefu wa jengo la utawala ambalo huwafanya walimu wa shule ya Mandewa mpaka sasa kutumia darasa kama ofisi kwa shughuli za uwajibikaji.

“Tuna ukosefu huo wa jengo la utawala, maktaba, upungufu wa nyumba za walimu, upungufu wa fedha za ujenzi wa bweni kiasi cha shilingi milioni hamsini, pia hatuna hostel kwani wanafunzi wengi wanatembea umbali mrefu wa takribani kilometa 10 kutoka maeneo ya Mwaja, Uhamaka, Ititi na maeneo mengine hadi kufika eneo la shule…hali hii huwalazimu baadhi ya wazazi kuwapangishia vyumba watoto jambo ambalo linahatarisha maisha hasa kwa watoto wa kike,” alisema Maghiya. 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: