Raisa Said ,Tanga
IMEELEZWA kuwa Maambukizi ya Virus vya Ukimwi (VVU) kwa watoto wenye umri wa kuanzia Miaka 0-5 imepungua kutokana na elimu inayoendelea kutolewa katika Jiji la Tanga.
Kwa Mujibu wa Mratibu wa Ukimwi Jiji la Tanga Moses Kisibo alisema kuwa elimu katika makundi mbalimbali ikiwemo kwa wajawazito imesaidia kupungiza Maambukizi katika kundi hilo la watoto wadogo.
Kisibo alisema kuwa kwasasa kundi ambalo ni changamoto ni kundi la watoto wenye umri wa Miaka I5 - 35 nakwamba ndilo kundi linaloongoza kwa Maambukizi mapya ambapo kitaifa ni asilimia 40.
Alisema ili kupambana na kundi hilo ni lazima elimu iendelee kutolewa kwa jamii ikiwa ni pamoja na Wazazi kujenga mahusiano ya karibu na watoto wao ili wanapofanyiwa ukatili inakuwa rahisi kuwapatia taarifa.
Katika maadhimio ya siku ya Ukimwi yaliyofanyika Dec 1 ,Kimkoa Wilayani Muheza ,Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema kuwa lengo la Kitaifa na Kidunia ni Ifikapo mwaka 2030 kuhakikisha wanatokomeza Maambukizi mapya ya ugonjwa wa Vvu na Ukimwi.
Katika kuhakikisha lengo hilo linatimia amesema ni lazima kuvunja mtandao wa ngono zisizo salama katika makundi hatarishi jambo ambalo litasaitia pia kuzunguza vifo vitakanavyo na Vvu na ukwimwi.
Malima amewataka watumishi wote wa Idara ya Afya walipo katika Halmashauri 11 za Mkoa wa Tanga kuhakikisha wanaendelea na uhamasishaji, utoaji wa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kupima na kujua afya zao.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa huyo alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kuacha kunyanyapaa na kubagua wagonjwa wanaoishi na ugonjwa huo ambao ni hatari kwa jamii.
Mwisho
Post A Comment: