Meneja wa Benki wa  Benki ya CRDB PLC Kanda  Kaskazini Chiku Issa (kushoto) kwa niaba ya Mkurugenzi wa benki hiyo Tanzania akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja moja ya mfuko wa saruji nyeupe kati ya 116 yenye thamani ya Sh. milioni 5  kwa ajili ya kukarabati Hospitali ya Tumaini ikiwa ni kkuunga mkono wiki ya Maendeleo Wilayani Hanang' 

Mkuu wa Wilaya ya Hanang akizungumza wakati akipokea msaada huo..
Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Hanang wakiwa kwenye makabidhiano hayo.
Makabidhiano ya saruji hiyo yakiendelea. 


Na Dotto Mwaibale, Hanang'


MKUU wa Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara, Janeth Mayanja amepokea saruji nyeupe mifuko 116 yenye thamani ya Sh.5,000,000 iliyotolewa na Benki ya CRDB PLC Kanda  Kaskazini  kwa ajili ya  kusaidia kukarabati Hospitali ya Tumaini wilayani humo.

Saruji hiyo ilikabidhiwa na Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kaskazini Chiku Issa kwa niaba ya Mkurugenzi wa benki hiyo Tanzania kwa ajili ya kuunga mkono wiki ya Maendeleo Wilayani Hanang' Iliyofanyika   kuanzia Novemba 1, 2021 hadi Novemba 5, 2021 kufuatia benki hiyo kuwa na ratiba zingine.

Akikabidhi mchango huo Bi Chiku Issa  alisema fedha zilizotumika kununulia saruji hiyo zimetokana na faida waliyoipata na ndio maana wakaona warejeshe sehemu ya faida hiyo kwa jamii ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita hasa katika kugusa Sekta ya Afya kwa kuchangia ukarabati wa Hospitali hiyo iliyojengwa kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye,  Mama Ester Sumaye kupitia Taasisi ya Hope Foundation.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya hiyo Janeth Mayanja ameishukuru benki hiyo ya kwa mchango wao huo na amewaahidi kuendelea kutoa ushirikiano wake kwa benki hiyo na zingine zote zinazotoa huduma katika wilaya ya Hanang' kwa maslahi mapana ya wananchi.

Aidha Mayanja amezihizimiza kampuni/Taasisi za Kibiashara  za wilayani humo kuendelea kutoa sehemu ya faida walizopata katika kuboresha huduma za afya na elimu.

Mayanja alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchiwote wa ndani  na nje ya wilaya hiyo pamoja na wadau mbalimbali ambao hawakuweza kushiriki wiki ya maendeleo na wana nia ya kushiriki   kuendelea kuchangia.

Hafla hiyo ya Disemba 7, 2021 Ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na chama,wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Usalama ,Mkurugenzi Wa Halmashauri Jennifa Omolo ambaye aliambata na wakuu wa Idara, CHMT, Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Wilaya ya Hanang'  Mathew Darema ambaye aliambatana   na Kamati ya Siasa ya Wilaya pamoja na makatibu wa CCM kutoka kata zote na wakuu wa taasisi  mbalimbali.


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: