Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo (kushoto) akisisiizia jjaambo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy pamoja na baadhi ya wakandarasi na watumishi wa TANESCO mara baada ya kutembelea mradi wa REA unaendelea kuunganisha kwenye maeneo ya Dagaza Bagamoyo mkoa wa Pwani. Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo akizungumza na wakandarasi wa Mradi wa REA wilayani Bagamoyo (hawapo pichani) kujadili ni namna gani wanaweza kukamilisha mradi wa REA wilayani humu.Kikao hicho kimaekaa leo Tarehe 27/11/2021. Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) akizungumza na wakjandarasi wa Mradi wa REA wilayani Bagamoyo (hawapo pichani) kujadili ni namna gani wanaweza kukamilisha mradi wa REA wilayani humu.Kikao hicho kimaekaa leo Tarehe 27/11/2021.


Wakandarasi wilaya ya Bagamoyo wakifuatilia kikao ambacho walikaa na uongozi wa mradi wa REA kujadili akizungumza na wakjandarasi wa Mradi wa REA wilayani Bagamoyo (hawapo pichani) kujadili ni namna gani wanaweza kukamilisha mradi wa REA wilayani humu.Kikao hicho kimaekaa leo Tarehe 27/11/2021.Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (kulia) pamoja na baadhi ya wakandarasi na watumishi wa TANESCO mara baada ya kutembelea mradi wa REA unaendelea kuunganisha kwenye maeneo ya Dagaza Bagamoyo mkoa wa Pwani.


Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy pamoja na baadhi ya wakandarasi na watumishi wa TANESCO mara baada ya kutembelea mradi wa REA unaendelea kuunganisha kwenye maeneo ya Dagaza Bagamoyo mkoa wa Pwani.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEEL MBATILO)


******************************


NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO PWANI


Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo amewataka wakandarasi ambao wanasimamia mradi wa kuunganisha Umeme Vijijjini kutengeneza mpango kazi kuanzia sasa mpaka muda watakaokabidhi mradi kutegemea unaisha lini ili kuweza kurahisha na kumalizka kwa mradi kwa wakati.


Ameyasema hayo leo tarehe 26/11/2021 wakati alipokutana na wakandarasi wa Wilaya ya Bagamoyo ambao wanasimamia uunganishaji wa umeme katika ameneo hayo na kueleza changamoto zinazokwamisha ukamilishaji wa mradi kwa wakat.


"Kuna miradi inakwisha tarehe 31 Desemba mwaka huu na kuna miradi ambayo itakwisha tarehe 31, Desemba mwaka kesho na hiyo mipango kazi yenu iwe ina muda maalumu wa kuelekeza". Amesema Wakili Kalolo


Aidha Wakili Kalolo amewaelekeza wakandarasi hao kuwa na mahusiano mazuri na kule wanapotoa huduma kwanza kwa kujitambulisha kwa viongozi wa Mkoa,Wilaya na Vijijini pia kuwepo na ushirikiano kuanzia ngazi ya chini ili kupata vibarua wa kuwasaidia kufanya kazi hizo.


Pamoja na hayo amewahimiza viongozi wa Serikali kuhakikisha wanahamasisha ulinzi wa miundombinu hiyo ili iendelee kuleta tija kwa watumiaji wa mwisho.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema mradi huo ulitakiwa uunge vijiji maeneo 227 na mpaka sasa maeneo 226 yameshaungwa bado eneo moja ambalo baada ya kukagua wakaona miundombinu upande wa TANESCO haijafika kutokana na miundombinu ya mkandarasi .


Amesema mpaka sasa mradi unaenda vizuri toka uanze mpaka sasa kati ya wateja 37,000 wa awali ambao walitakiwa waunganishiwe sasa hivi wateja 33,500 wameshaunganishiwa.


Nae Mjjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Bw.Aswald Urassa amesema ni muhimu wakandarasi kuheshimu mikataba na kufanya kazi ndani ya mkataba na hakutakuwa na muda wa nyongeza kama muda wa mkataba ukiisha.


Kwa hattua nyingine, Mandarasi wa Mradi Mhandisi Alfred Kessy amesma ongezeko la watu ambao huitaji kuunganishiwa huchangia kwa kiasi kikubwa kuchelewa kumalizika kwa mradi huo.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: