Mkurugenzi wa Mipango  Mikakati na Ubunifu wa Taasisi ya Bahari Safi, Omari Mbwana (kulia) akiwa katika moja ya mkutano wa kuendeleza Fukwe ya Coco. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe.
Mkurugenzi wa Mipango  Mikakati na Ubunifu wa Taasisi ya Bahari Safi, Omari Mbwana (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe katika moja ya mkutano wa kuendeleza Fukwe ya Coco. 


Na Mwandishi Wetu


TAASISI ya Bahari Safi yenye makao yake makuu jijini Dar esSalaam ambayo inajishughulisha na uhamasisha jamii juu ya utunzaji wa Bahari imesema kila mtu anajukumu la kusimamia usafi katika Bahari.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mipango  Mikakati na Ubunifu wa Taasisi hiyo Omari Mbwana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli wanazozifanya.

"Lengo la kuwaiteni hapa leo ni kutaka kuwaomba kufikisha ujumbe kwa wananchi ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa na jukumu la kusimamia usafi katika Bahari".alisema Mbwana. 

Alisema jukumu kubwa la taasisi hiyo ni kutoa hamasa kwa wananchi kuona umuhimu wa utunzaji wa mazingira baharini ili kulinda samaki na viumbe hai wengine waishio humo.

Alisema kwa kipindi kirefu baada ya kufanya tafiti kadhaa wamebaini kwamba uchafuzi wa mazingira baharini unafanywa na baadhi ya watu ama jamii inayotumia bahari kwa shughuli mbalimbali zikiwemo uvuvi wasafiri.

Alisema kutokana na changamoto hizo waliona ni vema kupitia taasisi hiyo kupaza sauti kwa jamii ili kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na  kuachana na tabia ya kutupa taka, kumwaga sumu kwa ajili ya kuvua samaki jambo ambalo ni hatari kubwa kwa maisha ya samaki,  viumbe wengine na walaji wa samaki.

Mbwana alisema ili kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa wanataraji kutoa elimu kwa watumiaji wa bahari wakiwemo wasafiri na wavuvi ambao baadhi yao hawajui  kutunza mazingira ya baharini jambo litakalo saidia mazalia ya viumbe hai wakiwemo samaki wanakuwa salama wakati wote kama walivyo viumbe wengine waishio duniani.

"Viumbe hai wa baharini wana haki ya kuishi kama viumbe wengine hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kwa ngazi mbalimbali kuchukua jitihada za makusudi kupambana na vitendo vya baadhi ya watu au jamii za kuchafua mazingira ya baharini kwa kutojua au kwa bahati mbaya wakati wanapoitumia kwa namna moja hama nyingine".alisema Mbwana.


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: