Jane Edward, Arusha


Wananchi waishio pembezoni mwa hifadhi za wanyama na maliasili wametakiwa kuchukua tahadhari ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo mabadiliko hayo yamekuwa yakileta changamoto kati ya binadamu na wanyama.Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Longido wakati akifungua warsha ya wadau wa mradi wa mabadiliko ya tabia ya nchi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela,


Ambapo alisema  mabadiliko ya tabia ya nchi yamekua ni changamoto kubwa kwa maisha ya binadamu na maendeleo ya kiuchumi ya mtu mmoja mmoja na na nchi kwa ujumla.


Aliongeza  kuwa watu wamekuwa wakiuawa na wanyama pori na Ni wiki chache walipokea taarifa za kuuawa kwa mwanakijiji wilayani Same lakini pia wameshuhudia mifugo ikifa pamoja na mazao kuharibiwa vibaya na wanyama pori na yote hayo yanasababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.


“Wanyama wanakosa maji na chakula porini jambo linalosababisha wanasogea karibu na makazi ya watu lakini nao binadamu kwa kutafuta ardhi yenye rutuba kwaajili ya kilimo na mifugo wanajikuta wanasogea zaidi karibu na maeneo ya hifadhi jambo linaloleta muingiliano na migogoro Kati ya binadamu na wanyama pori,” Alisema Babu


Alisema kuwa mradi wa mabadiliko ya tabia ya nchi umewezesha ujenzi wa malambo ambao utasaidia kupunguza muingiliano kati ya binadamu na wanyama hasa pale yanapopatikana maji ya kutosha kwaajili ya wanyama pori na mifugo ambapo zimetengenezwa pampu za maji zinazotumia umeme wa jua, wameweka uzio kuzuia wanyamapori kuvamia maeneo ya makazi na mashamba.


“Mradi huu umetekelezwa kwa muda mfupi na ipo katika kiwango kinachokidhi vigezo na mahitaji na kwakweli binafsi na kwa niaba ya serikali niwashukuru kwa kujitolea katika kukamislisha kazi hii nafahamu wapo waliofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mradi unakamika,” Alisema.Aidha aliwaagiza wananchi waliopo katika maeneo ambayo miradi hiyo imetekelezwa kuhakikisha wanatunza miradi hiyo na  kukidhi malengo yaliyokusudiwa kwani WWF wamewasaidia lakini hawategemei warudi kuja kusimamia miradi hiyo kwani kwa sasa ni yakwao hivyo wailinde,waihudumie na kuitunza ili iwasaidie kupunguza makali ya mabadiliko ya tabia ya nchi.


Alisema kuwa mradi huo unafikia mwisho lakini bado wanahitaji msaada mwingine katika kuhakikisha wanaibua miradi mingine ili wananchi weweze kunufaika lakini kwa wakati mwingine hizi WMA zisimame zenyewe kusiwe na visingizio kwani jamii nyingi zinategemea maliasili kiuchumi na kimaendeleo.kwa upande wake meneja wa mradi huo Novat Kessy alisema  mradi huo unatekelezwa na shirika la uhifadhi wa mazingira (WWF) ambapo wamefanya mradi huo ili kuzijengea jamii uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo katika maeneo ya Kaskazini madhara makubwa Ni ukame na wamekuja na mkakati wa kuwewezesha kukabiliana nayo.


Alisema jamii wanazofanya nazo kazi Ni wafugaji na wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata maji ambapo wamewasaidia kwa kuwajengea mabwawa makubwa(Malambo) kwani wamekuwa wakipata mvua chache na ili maji yake yasipotee mabwawa hayo yanatumika kwa kuhifadhia maji yatayotumika wakati wa ukame.


Sambamba na hayo pia tunazijengea jumuiya za wanyapori za uhifadhi za kijamii uwezo wa kupanda miti pamoja na kuwapa mafunzo ya malisho yanayokabiliana na ukame ambapo wamepewa mbegu za malisho na mradi huu unafadhiliwa Ujerumani ambapo mradi umetekelezwa kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi


Kwa upande wake Profesa Noah Sitati mtaalamu wa masuala ya wanyama pori alisema kuwa hadi sasa Kuna maji katika maeneo yote ambayo wamefanyia mradi huo uliogharimu URO milioni 5.2 kwa Tanzania na Kenya ambapo Tanzania wamenufaika kwa asilimia 51 na Kenya kwa asilimia 49.


 Alifafanua kuwa kwa kumalizika kwa mradi huo umepelekea kuanzishwa kwa mradi mwingine wa miaka mitatu utakaoanza January 2022 ambao utahusika na masuala ya Tembo na mradi huo unaanziswa mahususi kutokana ongezeko kubwa la idadi ya tembo na utagharimu URO milioni 10.2 ambapo pia utatekelezwa Kenya matumizi ya kwa asilimia 49 na Tanzania kwa matumizi ya 51.

Share To:

Post A Comment: