Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akionesha manjonjo kwa kucheza muziki katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Oktoba 28 hadi 30, 2021 katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TASUBA) mjini Bagamoyo.Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.Zainab Abdallah akionesha manjonjo kwa kucheza muziki katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Oktoba 28 hadi 30, 2021 katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TASUBA) mjini Bagamoyo.


Msanii wa Taarabu Isha Mashauzi akitumbuiza katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Oktoba 28 hadi 30, 2021 katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TASUBA) mjini Bagamoyo. Msanii wa Kizazi kipya Beka Flaver akitumbuiza katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Oktoba 28 hadi 30, 2021 katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TASUBA) mjini Bagamoyo.

***********************************
NA MWANDISHI WETU, BAGAMOYO


Wasanii wa Bongo Fleva na Muziki wa Taarabu jana, Oktoba 28, 2021 wamekiwasha wakati wa Tamasha la 40 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni lililozinduliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa katika viwanja vya TaSuBa mjini Bagamoyo.

Wasanii hao wamewakosha wadau mbalimbali na viongozi kwa ufundi wao wa kuimba na kucheza.

Hali hiyo ilisababisha kuwanyanyua baadhi ya viongozi waliohudhuria tamasha hilo akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi ambaye alikuwa miongoni wa kivutio kikubwa kutokana na umahili wake wa kucheza na kuchana misitari.

Ikumbukwe kuwa wakati akiwatambulisha wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha hilo la Kimataifa kwa Waandishi wa Habari Oktoba 26, 2021 Dkt. Abbasi alisema katika Tamasha hili ataongoza Wasanii wa Hiphop kudadavua mistari

Wasanii waliotumbuiza ni Beka Flavour, Isha Mashauzi, Saada Nassor kutoka Zanzibar, Saraphina na Ruby.

Tamasha hilo linaendelea leo Oktoba 29, 2021 na linatarajiwa kufikia kilele hapo kesho Oktoba 30, 2021.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: