Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Ludewa Adrea Tsere mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Ludewa ukitokea mkoa wa Ruvuma.

Mwenge wa uhuru ukiwa kwenye mradi wa mjasiliamali wa ufugaji wa Samaki na Ng’ombe katika mtaa wa Magoda halmashauri ya mji wa Njombe.

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

WANANCHI mkoani Njombe wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria ili waendelee kuwa na afya ambayo itawasaidia kujishughulisha na kazi  ambazo zitachochea kukuza uchumi wao  na taifa kwa ujumla.


Wito huo umetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi wakati wa zoezi la ugawaji vyandarua kwa zaidi ya watoto yatima 100 na kadi za Bima ya Afya wa kituo cha Imiliwaha Halmashauri ya Mji wa Njombe ambapo amesema kuwa licha ya kuwa ugonjwa wa malaria ni hatari lakini unaweza kuepukika kwa wananchi kwa kuchukua tahadhari ya kusafisha mazingira.


“Tunaendelea kukupusha kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya kauli mbiu isemayo Ziro Malaria inaanza na mimi nachukua hatua kuitokomeza.Uhonjwa wa Malaria bado upo na unaendelea kutesa jamii zetu hasa watoto,wajawazito na jamii kwa ujumla hivyo tunakumbushwa kuchukua tahadhari ikiwemo kufanya usafi katika maeneo yanayotuzunguka lakini pia kulala kwenye vyandarua vyenye viwatilifu”alisema Josephine Mwambashi


Awali akisoma taarifa mbele ya kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji wa Njombe Julius Mbata Amesema Jumla ya Vyandarua 150 Vimetolewa kwa watoto yatima wa Kituo Cha Imiliwaha.


“Aidha sekta binasi imehamasishwa kufungua maduka ya kuuza dawa amabpo kwa mwaka 2020 kulikua na maduka 107 kati yao maduka matano yalikuwa yanauza vyandarua na mwaka 2021 idadi imeongezeka na kufikia maduka 7 yanayouza vyandarua”alisema Julius Mbata

 

Akipokea mwenge wa uhuru kutoka wilaya ya ludewa,Mkuu wa wilaya ya njombe Kissa Kasongwa amesema  kuwa katika wilaya yake  jumla ya miradi 11 yenye thamani ya zaidi bilioni mbili itapitiwa na kuzinduliwa na mwenge huo.


“Mwenge wa uhuru katika wilaya ya Njombe utakimbizwa KM 157.8 ambao jumla ya miradi 11 yenye thamani ya shilingi bilioni mbili milioni mia saba themenini na tisa,laki tisa thelathini na saba. utapitiwa kati yake miradi mitatu itazinduliwa,mine itakaguliwa,miwili itawekewa mawe ya msingi na mmoja wa kukabidhi hundi kwa watu wenye ulemavu “alisema Gwakisa


Hata hivyo miradi yote iliyopitiwa na mwege wilayani humo Imepitiwa na kukubaliwa na kiongozi wa mbio za mwenge huku akiridhiswa na miradi hiyo licha ya kusisitiza kuongeza umakini katika ujenzi na matumizi ya fedha kwenye miradi mbali mbali ya serikali.

Share To:

Post A Comment: