Na. Angela Msimbira MROGORO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini kuiga mpango wa kuwapanga wamachinga uliofanywa na Mkoa wa Morogoro lengo likiwa ni kuwapanga kwa kuwapatia maeneo mazuri ya kufanyia biashara
Ametoa maagizo hayo leo wakati akizundua vibanda vya wafanyabiashara wadogo (wamachinga) uliofanyika katika soko la chifu Kingalu, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkoani Morogoro
Waziri Ummy ameupongeza Mkoa wa Morogoro kwa kuwa wa kwanza katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani alilolitoa kwenye mkutano wa vijana Jijini Mwanza mnamo tarehe 15/6/2021 hivyo amewaagiza Mikoa mingine kujifunza na kuhakikisha wanatekeleza maagizo kwa wakati ili kuwapunguzia adha wamachinga ambao wanapata changamoto katika kufanya bishara zao.
Ameendelea kufafanua kuwa dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka imeelekeza kujenga uchumi unaoakisi hali halisi ya Mtanzania kwa kukuza viwanda vidogo na vya kati hivyo ili Tanzania ifike na kukua kiuchumi wafanyabiashara wadogo lazima kuwa sehemu muhimu ya kukuza uchumi wa nchi
Waziri Ummy wafanyabiasha wadogo ni muhimu katik kukuza uchumi wan chi, hivyo ni muhimu tukawadhamini na kuwajali kwa kuwawekea mazingira bora ya kufanyia bishaara kwa kuwatengea maeneo yaliyobora katika Halmashauri zote nchini
Ameagiza Mikoa yote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya kuwapanga wamachinga ambao wengi hujishughulisha katika maeneo ambayo si rasmi na hayana usalama katika biashara zao
Aidha , amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassani itaendelea kudhamini, kuheshimu na kukuza shughuli za wafanyabiashara wadogo wakiwemo wamachinga
Mkoa wa Morogoro unakadiriwa kuwa na wamachinga 781 ndani ya Mitaa ya mijini waliotambuliwa katika mpango maalum wa kuwapanga wamachinga Mkoani hapo
Post A Comment: