Mratibu wa Utafiti na Machapisho kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Mkuu wa Mradi wa UMFULA Prof. Japhet Kashaigili (Wa Kwanza Kulia) akimkabidhi Flash Disc yenye matokeo yote ya Utafiti huo wa miaka mitano Mkurugenzi wa Bodi ya Maji  Bonde la Rufiji Mhandisi Florence Mahay kwa ajili ya kuyatumia kwa shughuli mbalimbali za uhifadhi wa Bonde na pia nyingine kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.


Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji Mhandisi Florence Mahay akieleza faida za Matokeo ya utafiti huo katika Ustawi wa Bonde la mto Rufiji.(Mweye suti ya Blue).

Mratibu wa Utafiti na Machapisho kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Mkuu wa Mradi wa UMFULA Prof. Japhen Kashaigili akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Matokeo ya utafiti huo mara baada ya kumaliza kuyawasilisha kwa wadau wote waliohudhuria kwa njia mbalimbali duniani ikiwemo Zoom.

Picha ya pamoja ya baadhi ya Wadau walioshiriki Mkutano huo wa kupokea matokeo na kufunga Mradi huo wa utafiti wa UMFULA uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji Mjini Iringa.
Picha zingine ni Wadau wakifuatilia Uwasilishwaji wa matokeo hayo uliofanywa na watafiti mbalimbali ukumbini hapo na wengine waliowasilisha kwa njia ya mtandao yaani ZOOM.
Picha zingine ni Wadau wakifuatilia Uwasilishwaji wa matokeo hayo uliofanywa na watafiti mbalimbali ukumbini hapo na wengine waliowasilisha kwa njia ya mtandao yaani ZOOM.
Picha zingine ni Wadau wakifuatilia Uwasilishwaji wa matokeo hayo uliofanywa na watafiti mbalimbali ukumbini hapo na wengine waliowasilisha kwa njia ya mtandao yaani ZOOM.
Picha zingine ni Wadau wakifuatilia Uwasilishwaji wa matokeo hayo uliofanywa na watafiti mbalimbali ukumbini hapo na wengine waliowasilisha kwa njia ya mtandao yaani ZOOM.
Picha zingine ni Wadau wakifuatilia Uwasilishwaji wa matokeo hayo uliofanywa na watafiti mbalimbali ukumbini hapo na wengine waliowasilisha kwa njia ya mtandao yaani ZOOM.


Na Calvin Gwabara, Iringa


WADAU wa Bonde la Mto rufiji wametakiwa kuendelea kujizatiti katika kudhibiti shughuli za kibinadamu ambazo zinachangia katika kuharibu mtiririko wa maji ili kuepukana na athari zinazoweza kutokea na kuathiri mahitaji ya maji ya wadau wote wanaotegemea maji hayo.

Wito huo umetolewa na Prof. Japhet Kashaigili ambaye ni Msimamizi na Mratibu wa Mradi wa utafiti wa kutathimini ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye bonde la mto Rufiji na kuangalia athari zake katika mtiririko wa maji na utengenezaji wa vielelezo vya kusaidia kupanga mipango ya kimaendeleo katika bonde hilo (UMFULA) wakati wa Mkutano wa kuwasilisha matokeo ya mwisho ya Utafiti huo na kufunga mradi.

“ Kutumia Modeli 34 zinazotumiwa na IPCC zimeonesha kuwa mfumo wa mvua ni wa kubadilika sana na kwamba huko mbeleni kunaweza kuwepo kwa mvua nyingi au mvua chache hasa kwenye maeneo ya kusini mwa Bonde hilo hivyo taarifa hizi zinaisaidia nchi katika kujipanga ikitokea mvua zimeongezeka nini kifanyike na zikipungua nini kifanyike na hivyo mradi umeainisha mambo ya kufanya katika hayo yote” Alifafanua Prof. Kashaigili.

Aliongeza “ Lakini kubwa kabisa tunaangalia Mvua ikipungua nini kifanyike maana sasa hivi tunatambua nchi ipo katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile Mradi wa umeme wa Mwl Nyerere ( JNHPP) hivyo ni lazima kuwe na mipango ya kuhakikisha kunakuwa na maji ya kutekeleza mradi huo ili uweze kuzalisha umeme kama ulivyopangwa hivyo Modeli hizo zinazoonyesha kunaweza kuwa na upungufu wa mvua zinatupa kiashiria cha kuweza kujipanga zaidi”.

Amesema kuwa pamoja na matokeo hayo ya kupanda au kushuka kwa mvua lakini matokeo ya jumla yanaonesha kuna kila sababu ya wadau wote kujipanga katika kukabiliana na hali hiyo hasa kutokana na viashiria vikubwa kabisa kuonesha vinatokana na shughuli za kibinadamu hasa maeneo ambayo kuna ukataji mkubwa wa miti.

“Tumeona maeneo yaliyokatwa miti sana mvua zikinyesha maji yanakaa kwa muda mfupi na kukauka na hii maana yake ni kwamba kipindi cha kiangazi ambapo maji yanahitajika kuwepo ili kutunza baionuai kwenye  mito na kuwezesha mabwawa kuendelea kupata maji yanayoingia kupungua hivyo jitihada lazima zifanyike ili kuendeleza mtiririko huo wakati wote kwa kutunza maeneo yote ya bonde.

Mratibu na Msimamizi huyo wa Mradi huo wa Utafiti upande wa Tanzania ameongeza kuwa kupitia Modeli hizo wameona pia kuwa kuna uzalishaji mkubwa wa mchanga unaoingia kwenye maeneo ya mabwawa kwa sababu maeneo mengi ya dakio hilo au Bonde yenye ardhi oevu ambazo husaidia kupunguza  mchanga usiende kwenye mabwawa zimelimwa na kubadilishwa matumizi hivyo utafiti huo pia umeeleza kinachopaswa kufanyika ili kunusuru mabwawa ya kuzalisha Umeme kujaa mchanga.

Prof. Kashaigili amesema matokeo mengine waliyoyapata ni kwenye kuangalia upunguaji wa maji kwa sasa na tangu kuanzishwa kwa vituo vya kupimia maji miaka 40 iliyopita wamebaini kuwa mabadiliko sio makubwa lakini tofauti inaonekana wakati wa kiangazi kwamba maji yanaendelea kupungua kadri siku zinazoenda hali ambayo haikuwepo zamani nankiashiria kikubwa na hali iliyopo sasa kwenye Mto Ruaha Mkuu kukauka Mara kwa mara kuanzia miaka ya 1990.

“ Pia swala la ugawaji wa maji ni swala muhimu ambalo linahitaji kuwa na vifaa maalumu wa kuwezesha kufanya ugawaji kwa usahihi na Mradi umeweza kutengeneza Modeli nzuri na ya kisasa ambayo itapatikana kwenye mtandao na hii itasaidia watu wa Bonde kugawa maji kwa utaratibu mzuri ili kupunguza changamoto za ugawaji wa maji bila kufanya tathimini kwanza na hii itasaidia maeneo mengi hata wizara na tutaendelea kuifanya iwe rahisi zaidi kutumia wadau” alieleza Prof. Kashaigili.

Akizungumzia faida za matokeo ya utafiti huo Mkurugenzi wa Bodi ya Maji  Bonde la Mto Rufiji Mhandisi Florence Mahay amesema yanawasaidia katika kufanya maamuzi na kupanga mikakati ya namna ya kutekeleza majukumu yao na kuwa na mipango endelevu ya matumizi ya Bonde hilo ambalo asilimia 80% ya umeme wa maji unategemea bonde hilo katika maji kuzalisha umeme.

“50% ya maeneo ya kilimo yanayomwagiliwa yapo katika bonde la mto Rufiji kwahiyo ni muhimu kujua kama upatikani wa maji katika maeneo hayo kutaathirika na mabadiliko ya tabia nchi basi ni kwa namna gani na kiasi gani na hasa hayo mabwawa ambayo yakikosa maji yataathiri uchumi wa nchi sambamba na maeneo yaliyohifadhiwa kama vile hifadhi za taifa” Alisema Mhandisi Mahay.

Mkurugenzi huyo amesema changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni namna ya kuweka uwiano kati ya kilimo na miradi ya umeme kwani Miradi ya Umeme ipo chini wakati Kilimo kinafanyika juu ingawa Mradi wa umeme hauli maji kama kilimo bali ubayatumia tu na kuyaacha yatiririke lakini inazuia Miradi ya kilimo inayotumia maji ambayo ipo juu kutotumia maji hayo ili yafike kwenye mabwawa kwa wingi.

“ Tunaendelea sasa kuhamasisha Miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji ifanyike chini baada ya miradi ya Umeme ili kuweza kutumia maji ambayo yanatoka kwenye miradi ya umeme nankutiririka bila matumizi na kwenda Baharini hii itaongeza tija maana maji yanakuwa mengi yanakwenda bure au kutumiwa kidogo sana kwa kilimo” Alibainisha Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde Mhandisi  Florence Mahay.

Mradi huo wa miaka mitano umefanikiwa kusomesha wanafunzi kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu, Kutengeneza Modeli mbili pamoja na kuzalisha machapisho mbalimbali ya kisayansi na Majarida na Taarifa mbalimbali zkwa lugha rahisi kwaajili ya Wadau wote hasa Wakulima.


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: