Bwana harusi Victor Christopher akiwa na mkewe Cherly Mwaka baada ya kufunga ndoa yao katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Uharika wa Mtinko uliopo Wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida jana na kufuatiwa na sherehe iliyofanyika Ukumbi wa.Darabe uliopo eneo hilo la Mtinko.

Maharusi Victor Christopher na mkewe Cherly Mwaka (katikati) wakiwa na wapambe wao Elinuru Elisha na Anna Richard baada ya baada ya kufunga ndoa.
Bwana harusi Victor Christopher akiwasalimia wageni waalikwa waliofika kwenye sherehe ya ndoa yao
Baba na Mama wa Bwana harusi Mzee Christopher Philip Majii na Mke wake Josephine Mohamed Majii wakiwa kwenye hafla hiyo.

Wazazi wa Bibi harusi wakiwasalimia wageni waalikwa waliofika kwenye sherehe hiyo.
Ibada ya ndoa takatifu ikiendelea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mtinko.
Bibi na Babu wa Bwana harusi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanakwaya ya Kalvary wakitoa burudani kwenye sherehe ya ndoa hiyo.
Maharusi wakivikana pete.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mtinko, John Kibuga akitoa baraka kwa maharusi baada ya kufungisha ndoa hiyo.
Bwana harusi Victor Christopher akisaini shahada ya ndoa kabla ya kukabidhiwa.
Kaka wa Bwana harusi Charles Christopher akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Maharusi wakionesha shahada za ndoa baada ya kukabidhiwa.
Wanakamati ndogo ya sherehe hiyo kutoka Singida mjini wakifanya yao jukwaani kwenye sherehe hiyo.
Sherehe ikiendelea.
Maharusi wakikata keki.
Dada wa Bwana harusi Christina  Christopher (kulia) akiahidi kutoa kabati lenye thamani ya Sh.350,000 kwa mdogo wake ikiwa ni zawadi yake baada ya kuoa.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ndogo ya sherehe hiyo kutoka Singida mjini, Judith Ngussa akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Maharusi wakiwa na wajumbe wa kamati zote za sherehe hiyo.
Baba na Mama wa Bwana harusi Mzee Christopher Philip Majii na Mke wake, Josephine Mohamed Majii wakiwa wamejifunika kwa moja ya zawadi ya vitenge waliokabidhiwa kwenye hafla hiyo.

Wajumbe wa kamati ndogo ya sherehe hiyo kutoka Singida mjini wakiwa  kwenye sherehe hiyo.

Picha ya pamoja na maharusi.
Picha ya pamoja na maharusi.
Picha ya pamoja na maharusi.

Kwaito likiwa limekolea.

Kwaito limenoga.


Wanakwaya ya Kalvary wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi na mama wa Bwana Harusi (Aliyesimama kushoto kwa Bibi harusi).


Na Dotto Mwaibale, Singida. 

MCHUNGAJI John Kibuga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) Usharika wa Mtinko uliopo Wilaya ya Singida Vijijini amewataka vijana wanaingia kwenye ndoa kuwa na upendo kwa wake zao. 

Kibuga alitoa ombi hilo jana wakati akiwafungisha ndoa  Victor Christopher na Cherly Mwaka katika kanisa hilo baada ya kuamua kuwa mwili mmoja yaani mke na mume. 

"Ndoa sio majaribio bali inahitaji kuvumiliana na kusamehana pale mnapokoseana na si vinginevyo," alisema Mchungaji Kibuga. 

Alisema kijana anapoingia kwenye ndoa anakuwa ameingia kwenye majukumu ya kumlea mke wake  katika hali ya furaha na huzuni. 

Alisema vijana wengi wakishaoa tegemeo lao kubwa ni kupata mtoto na hasipopata migogoro ndani ya nyumba huanza jambo ambalo sio nzuri mbele ya jamii na mbele za Mungu kwani kupata mtoto ni majaliwa na isiwe sababu ya kuanza kunyanyasana. 

Alisema mtoto anatoka kwa Mungu hivyo kama wanandoa watakuwa na changamoto hiyo wajikabidhi mbele za Mungu kwani kwake hakuna linaloshindikana. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa sherehe za ndoa hiyo ndugu na baadhi ya viongozi wa dini waliwasihi wanandoa hao kuwa kitu kimoja kama walivyokula kiapo cha ndoa mbele ya madhabau ya Bwana. 

Walimtaka bwana harusi huyo kufanya kazi kwa nguvu na bidii ili nyumba yake isikose chakula na kuwataka kuvumiliana katika hali ya shida kwani maisha kuna kupata na kukosa. 

Waliwataka wanandoa hao kuwa na matumizi ya wazi ya simu zao kwani simu zimekuwa chanzo kikubwa cha mifarakano katika ndoa. 

Wazazi wote wa pande mbili waliwasihi watoto wao kwenda kuishi kwa upendo na kumtanguliza Mungu kwa kila jambo bila ya kusahau kusali.


               
Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: