Na John Walter-Babati.

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetakiwa kuhakikisha watu waliolipia kuunganishiwa umeme wanapatiwa huduma hiyo ndani ya muda mfupi ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.

Agizo hilo limetolewa leo Septemba 13, 2021 na mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange wakati akizungumza na Madiwani,Wenyeviti na Watendaji wa kata na vijiji katika tarafa ya Bashnet ikiwa ni ziara yake maalum inayolenga kuondoa malalamiko ya wananchi kuhusu nishati ya umeme huku akiambatana na wataalamu wa Tanesco katika kujibu hoja za viongozi hao.

Twange amesema amepata malalamiko mengi kutoka kwa watu waliolipia fedha kwa ajili ya kuunganishiwa umeme lakini hadi sasa hawajapata huduma hiyo.Aidha Mkuu wa wilaya amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo waliolipia Umeme pamoja na taasisi zote kuwa atasimamia watapatiwe huduma hiyo.

Akielezea kuhusu hilo kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Manyara Marcia Simfukwe amesema katika bajeti mpya ambayo itaanza kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu,maeneo na taasisi zote ambazo hazina umeme zitapatiwa huduma hiyo.Mkuu wa wilaya atafanya ziara hiyo katika tarafa zote za wilaya hiyo ambazo ni Babati,Bashnet,Gorowa na Mbugwe, na kote huko atazungumza na viongozi wa maeneo hayo.

Share To:

Post A Comment: