Waziri
wa Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa akizungumza
kuhusiana na mapinduzi ya Sekta ya Utangazaji pamoja na Mfumo wa Uombaji
leseni kwa njia ya Mtandao utapolea mapinduzi makubwa nchini.
Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile pamoja na
Waziri wa Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wakiwa
katika uzinduzi wa Mfumo wa Uombaji leseni kwa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa utoaji wa leseni kwa njia ya
Mtandao wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika jijini
Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeanza kutumia Mfumo mwingine wa Maombi
ya leseni kwa kundi la leseni kubwa; mfumo huo unamuwezesha muombaji wa
leseni kuwasilisha maombi yake ya leseni kwa Mamlaka hiyo bila
kulazimika kufika ofisini na kukutana ana kwa ana na maafisa wa leseni.
Mfumo
huo laini wa maombi ya leseni (License Management System) unatarajiwa
kuzinduliwa siku ya Jumamosi Tarehe 31 Julai mwaka huu na Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile
(Mb) akiwa sambamba na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mheshimiwa Innocent Bashungwa Mawaziri ambao kwa pamoja wizara zao
zinasimamia sekta za Mawasiliano na Utangazaji kupitia Mamlaka ya
Mawasiliano (TCRA).
Mfumo huo mpya wa maombi ya leseni kupitia tovuti ya TCRA ambayo ni www.tcra.go.tz
utasaidia kuongeza ufanisi wa upatikanaji leseni kwa wateja wanaonuia
kutoa huduma za Mawasiliano na utangazaji, kurahisisha mchakato wa mteja
kupata huduma za leseni, utaokoa muda wa muombaji leseni, utaokoa
gharama za ufuatiliaji kwa mwombaji mpya wa leseni au anaetaka kuhuisha
leseni yake, utaongeza ufanisi kwa pande zote mbili yaani Mamlaka
inayotoa leseni na mwombaji, utaongeza uwazi kwa kuwa utamwezesha
mwombaji wa leseni kupata mrejesho moja kwa moja kwenye simu yake ya
kiganjani au kupitia barua pepe juu ya hatua zote na maendeleo ya
uchakataji wa leseni aliyoomba na kumwezesha Mwananchi kuendelea na
shughuli za maendeleo badala ya kufuatilia leseni.
Makundi
ya leseni yanayopatikana kwenye mfumo huu ambao mwombaji ataweza
kuwasilisha maombi yake bila kulazimika kufika katika ofisi za TCRA ni
pamoja na Leseni za pamoja ikihusisha leseni za Huduma ya Maudhui
(Content Services), Huduma ya Mtandao (Network Services), Huduma ya
Mifumo Tumizi (Application Services) na Miundombinu ya Mtandao (Network
Facilities).
Leseni
nyingine ni Leseni ya Huduma za Vifurushi na Vipeto, Leseni ya Mtumiaji
wa Masafa, Leseni ya Matengenezo na Usimikaji, Leseni ya Uagizaji Nje
na Usambazaji, Rasilimali za Utoaji Namba, Leseni ya Huduma za Posta kwa
Umma na Leseni ya Vifaa Vilivyoidhinishwa.
Hatua
ambazo mwombaji wa leseni husika atapaswa kufuata ni pamoja na
kutembelea tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ni www.tcra.go.tz
kisha kugonga kiunga cha Utoaji Leseni na kisha kubofya kiunga cha
Mfumo wa Kuomba leseni ambacho kitampeleka moja kwa moja kwenye ukurasa
wenye fomu za kujaza ili aweze kupatiwa leseni anayohitaji kwa ajili ya
kutoa huduma za Mawasiliano.
Hatua
za maombi ya leseni za Mawasiliano kwa kundi la leseni kubwa
(Individual License) zitasalia kama ilivyokuwa awali ambapo baada ya
mwombaji kuwasilisha maombi yake kupitia Mfumo wa Maombi ya Leseni,
itafuata hatua ya kutoa tangazo kwa umma kualika maoni ya wananchi juu
ya mwombaji leseni, kisha tathmini kufanyika juu ya ombi
lililowasilishwa, mwombaji kualikwa kutoa wasilisho la huduma ya
Mawasiliano anayotarajia kuitoa na kisha hatua ya uidhinishaji leseni na
hatimae mteja kupatiwa leseni.
Hatua
hii inakuja ikiwa ni mkakati wa serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania kurahisisha utaratibu wa upatikanaji huduma za leseni na
kuweka mazingira rafiki zaidi kwa wawekezaji katika sekta ya
Mawasiliano, sekta ambayo inatoa mchango chanya katika ukuaji wa
maendeleo ya taifa.
Post A Comment: