Staa
wa Simba, Clatous Chama jana jioni ameonja joto ya jiwe baada ya
kuchenjiwa kibao na muwekezaji wa klabu hiyo, Mo Dewji kisa Haji Manara.
Chama
akiwa Live Insta kwenye mkutano wake na mashabiki ambao Mo alikuwemo,
aliulizwa swali kuhusu kuondoka kwa Haji Manara ndani ya klabu ya Simba,
kwenye kujibu Chama alimsifia Haji kitendo ambacho kilionekana
kumchefua Mo.
Mo
alimuuliza Chama "Haji ndiye aliyekulipia ada ya uhamisho?" Chama akiwa
anamjibu Mo alijibu kwa kuomba msamaha kama amemkwaza, Mo akamuuliza
tena Nani aliyekulipa Ada....Haji? baadae Chama alipotaka kujibu Mo
akamwambia anatoka kwenye mkutano huo.
Hat
hivyo Chama amenukuliwa akisema "Kama Miquissone akiondoka, mimi pia
ikija ofa nzuri klabu ikakubali nitaondoka. Nimekaa Simba miaka mitatu,
nimefanya mambo mazuri, mashabiki wajue kuwa haya ni mambo ya kawaida
yanatokea. Nilishasema tangu awali kama muda ukifika na mimi nitaondoka
endapo ofa itakuja na Simba ikikubali,”.
Chama
ambaye amekuwa na mchango mkubwa kwa klabu hiyo tangu ajiunge nayo
mwaka 2018, aliongeza: “Ukitazama miaka yangu mitatu hapa Tanzania,
nadhani nimefanya vizuri kwa timu, ninauhakika mashabiki wanapaswa
kuelewa, endapo kuna klabu kubwa itajitokeza tutakaa na kujadili
tukikubaliana na Simba ikikubali nitaondoka.”
Kwa
misimu yote mitatu ambayo ameichezea Simba, Chama ameiwezesha klabu
hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu, huku ikibeba Kombe la FA mara
mbili mfululizo na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa
Afrika mara mbili.
Tayari
Simba ipo katika mipango ya kuboresha kikosi chake na imeshatangaza
usajili wa wachezaji wawili, winga Mmalawi Peter Banda pamoja na
mshambuliaji Yusuph Mhilu kutoka Kagera Sugar.
Mtendaji
Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, alimwambia mwandishi wetu kuwa, bado
wataendelea kutangaza usajili mpya kwa ajili ya kukiimarisha kikosi
hicho kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya ndani. “Kwa sasa
kazi yetu ni moja tu, kutangaza usajili, mambo mengine tunayaweka kando
kwanza,” alisema
Post A Comment: