Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza na kusambaza mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (wa pili kulia), akitoa maelekezo ya jinsi ya kujisajili katika App ya YaraConnect muda mfupi baada ya uzinduzi wake kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Wanaoangalia kutoka kushoto ni; Bwana Shamba Mwandamizi wa Yara, Maulidi Mkima, Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Yara, Deodath Mtei na Meneja Masoko, Sheila Chatto.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza na kusambaza mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (wa pili kulia), Bwana Shamba Mwandamizi wa Yara, Maulidi Mkima (kushoto), Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Yara, Deodath Mtei na Meneja Masoko, Sheila Chatto wakifurahia muda mfupi baada ya uzinduzi wa program maalumu iitwayo ‘YaraConnect APP’ kwa waandishi wa habari yenye lengo ya kutoa elimu ya kitaalamu kuhusu kilimo kwa wateja watakaojisajili jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza na kusambaza mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (kulia), akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa programu maalumu iitwayo ‘YaraConnect APP’ kwa waandishi wa habari yenye lengo ya kutoa elimu ya kitaalamu kuhusu kilimo kwa wateja watakaojisajili jijini Dar es Salaam leo. Wanaoangalia kutoka kushoto ni, Bwanashamba Mwandamizi wa Yara, Maulidi Mkima na Maneja Masuluhisho ya Kidigitali wa kampuni hiyo, Deodath Mtei.

Meneja Masoko wa Kampuni ya kutengeneza na kusambaza mbolea ya Yara Tanzania, Sheila Chatto (kulia), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuzindua programu maalumu iitwayo ‘YaraConnect APP’ yenye lengo ya kutoa elimu ya kitaalamu kuhusu kilimo kwa wateja watakaojisajili jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni; Bwanashamba Mwandamizi wa Yara, Maulidi Mkima, Mkurugenzi Mkuu wa Yara Tanzania, Winstone Odhiambo na Meneja Masuluhisho ya Kidigitaji, Deodath Mtei.

Bwanashamba Mwandamizi wa Kampuni ya kutengeneza na kusambaza mbolea ya Yara Tanzania, Maulidi Mkima (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa programu maalumu iitwayo ‘YaraConnect APP’ yenye lengo ya kutoa elimu ya kitaalmu kuhusu kilimo kwa wateja watakaojisajili jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake, Mkurugenzi Mkuu wa Yara Tanzania, Winstone Odhiambo, Meneja Masuluhisho ya Kidigitali, Deodath Mtei na Meneja Masoko, Sheila Chatto.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza na kusambaza mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (wa pili kushoto), Bwana Shamba Mwandamizi wa Yara, Maulidi Mkima (kushoto), Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Yara, Deodath Mtei na Meneja Masoko, Sheila Chatto (kulia), wakiwa katika mkutano wao na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuzindua programu maalumu iitwayo ‘YaraConnect APP’ yenye lengo ya kutoa elimu ya kitaalamu kuhusu kilimo kwa wateja watakaojisajili jijini Dar es Salaam leo.KAMPUNI ya kutengeneza na kusambaza mbolea ya Yara imezindua programu maalumu iitwayo ‘YaraConnect APP’ ikiwa na malengo ya kutoa elimu ya kitaalmu kuhusu kilimo kwa wateja wao watakaojisajili.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Yara Tanzania, Winstone Odhiambo alisema uzinduzi wa YaraConnect ni moja ya malengo yao katika kubuni mbinu sahihi za kitaalamu katika kilimo ikiwemo na njia ya kidijitali.

Alisema Yara ni kampuni inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa mbolea nchini Tanzania kwa takribani miaka 15 sasa ikiwa kampuni inayoongoza duniani katika uzalishaji na usambazaji wa mbolea ,utunzaji wa mazingira na kutoa suluhisho la kitaaluma kuhusu uzalishaji wa mazao mbali mbali.

“Hii ni App mpya kabisa itakayopatikana kwa kupitia simu za smart na inalenga wauzaji na wasambazaji wa bidhaa za Yara, watumiaji wa simu za android wataweza kupakua App hii kupitia Playstore na wale wa iOS (Iphone) watapakua kupitia Appstore”, alisema.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wasambazaji na wauzaji wa mbolea ya Yara wanaweza kutumia App hii kusajili biashara zao mara moja na kujizolea pointi kwa kupiga picha alama maalumu kutokana na manunuzi ya bidhaa za Yara huku wakipata taarifa kuhusu pointi zao na kutumia pointi hizo wanapotaka kujizolea zawadi zao mbali mbali kama Pikipiki, simu, pesa taslim na zawadi nyinginezo .

Aidha alisema wasambazaji pia watajifunza kupitia video za maarifa zipatikanazo ndani ya App na kujua maswali yanayoulizwa sana na wakulima wa eneo husika ambapo watumiaji watapata nafasi ya kupata msaada wa kitaalamu kuhusu lishe linganifu kwa mimea kupitia App hiyo.

“Napenda kuwafahamisha kuwa tutazindua App hii rasmi mwezi huu katika mikoa saba ya Tanzania bara ambayo ni pamoja na Kilimanjaro, Arusha, Tabora, Njombe, Mbeya, Iringa na Morogoro. Hivyo tunawakaribisha na kuwataarifu wasambazaji wa pembejeo kwa maeneo husika yakuwa ghafla hii siyo ya kukosa ili kuboresha huduma zao na kunufaika kipekee.

“Yara inatoa wito kwa wasambazaji wote wa bidhaa zetu wachangamkie fursa hii na tunaahidi kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, kuendelea kubuni mbinu nyingine za kidijitali zaidi ili kuhakikisha wadau wetu wanapata mafanikio mengi.

“Shughuli hii maalumu ya leo inatufanya Yara tuendelee kuwa mstari wa mbele katika masuala ya kilimo, mazingira na lishe hapa nchini Tanzania na duniani”, aliongeza Bwana Winstone.

Wateja na wadau wa Yara wanaweza pia kupata taarifa zaidi kupitia mitandao ya kijamii ya Instagram, facebook, twitter na youtube kwa kutumia jina yaratanzania.
Share To:

Post A Comment: