Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo akiongea wakati wa Mkutano na Wadau wanaosafirisha, kuingiza na kusambaza taka hatarishi katika ukumbi wa Millenium Tower jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kusikiliza changamoto za Wadau hao.
Sehemu ya Wadau wanaojishughulisha na biashara ya taka hatarishi. Amekutana na Wadau hao jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Millenium Tower ili kusikiliza maoni yao juu ya biashara hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakati wa kikao hiko kilichokutanisha Wadau wanaosafirisha, kuingiza na kusambaza taka hatarishi.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Andrew Komba akiongea wakati wa Mkutano wa Wadau wanaosafirisha, kuingiza na kusambaza taka hatarishi katika ukumbi wa Millenium Tower jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi NEMC Bi.Esnat Chaggu akizungumza wakati wa Mkutano na Wadau wanaosafirisha, kuingiza na kusambaza taka hatarishi katika ukumbi wa Millenium Tower jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kusikiliza changamoto za Wadau hao.
**********************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo amekutana na Wadau wanaojishughulisha na biashara ya taka hatarishi. Amekutana na Wadau hao jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Millenium Tower.
Amesema kuwa hivi karibuni
kumejitokeza changamoto nyingi katika kusimamia jukumu hilo na ameona ni
vyema akakutana na wadau wanaojihusisha na shughuli za kukusanya,
kusafirisha, kuhifadhi, kuingiza nchini, kusafirisha nje ya nchi na
urejelezaji wa taka hatarishi ikiwemo taka za kielekitroniki ili kwa
pamoja kuweza kujadiliana namna bora ya kukabiliana na changamoto hizo
na kutoa mapendekezo na maelekezo yatakayoimarisha usimamizi na udhibiti
wa taka hatarishi nchini.
Aidha aliongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa
kushirikiana na wadau ilifanya mapitio na kufanya marekebisho ya Kanuni
za Udhibiti wa Taka Hatarishi za Mwaka 2019 na kuandaa Kanuni mpya za
Udhibiti na Usimamizi wa Taka Hatarishi za Mwaka, 2021 (The
Environmental Management (Hazardous Waste Control and Management), 2019
na kufanya mapitio ya Kanuni za Ada na Tozo za Mwaka, 2019 na kuandaa
Kanuni za Ada na Tozo za Mwaka, 2021.
Pamoja na masuala mengine,
lengo kuu la kufanya mapitio ya Kanuni hizi lilikuwa ni kuweka mfumo
madhubuti wa usimamizi wa taka hatarishi nchini.
“Ikiwa ni takriban miezi miwili sasa tangu Kanuni hizi
zilipopitishwa mwezi Mei, 2021 na kuanza utekelezaji wake, nimeona ni
vyema pia tukumbushane matakwa ya Kanuni hizi na nyie wadau mtueleze
changamoto mnazokumbana nazo katika kuzingatia matakwa ya Kanuni husika
ili sote kwa pamoja tuweze kuimarisha usimamizi wa taka hizi”.
Pia alitumia wasaa huo kuwakumbusha Wadau hao kuwa Tanzania imeridhia Mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo inatoa fursa ya ushirikiano wa kimataifa katika kusimamia na kudhibiti usafirishaji wa taka hatarishi baina ya nchi na nchi.
Miongoni mwa Mikataba hiyo ni
Mkataba wa Basel unaosimamia udhibiti wa usafirishaji wa taka hatarishi
kutoka nchi moja na kwenda nchi nyingine na Mkataba wa Bamako unaozuia
uingizaji na usafirishaji wa taka hatarishi ndani ya Afrika ambayo yote
kwa pamoja tuliridhia mnamo mwaka 1993.
Katika kutekeleza matakwa ya Kanuni mpya za Udhibiti na
Usimamizi wa Taka Hatarishi za Mwaka, 2021 (The Environmental Management
(Hazardous Waste Control and Management), na Utekelezaji wa Mikataba ya
Kimataifa tuliyoridhia kumekujitokeza changamoto mbalimbali. Miongoni
mwa changamoto hizo ni pamoja na: Baadhi ya wadau kuingiza nchini Taka
hatarishi bila kupata idhini kutoka Mamlaka za Nchi ambayo Shehena
inatopotoka na inapoingia, Baadhi ya wadau kuchelewa kuhuisha vibali na
hivyo kupelekea usumbufu katika uendeshaji na usimamizi wa shughuli za
ukusanyaji, uhifadhi na usafirishaji wa Taka hatarishi, Baadhi ya wadau
kutokuwasilisha taarifa za viwango vya taka hatarishi
walivyokusanya/hifadhi/kusafirisha kama inavyoelekezwa katika kanuni za
taka hatarishi za mwaka 2021 (Ripoti ya kila nusu mwaka), Baadhi ya
wadau kutowasilisha nyaraka sahihi na kwa wakati na hivyo kusababisha
ucheleweshaji katika utoaji wa vibali, Baadhi ya wadau kutokufuata
utaratibu katika kufuatulia vibali vyao ikiwemo kufuatilia vibali moja
kwa moja Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira bila kupitia Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Baadhi ya wadau ya wadau hususan
wanaojishughulisha na shughuli za ukusanyaji, uhifadhi na usafirishaji
wa Chuma chakavu kuhujumu miundo mbalimbali nchini.
Alimalizia kwa kusema kuwa pamoja na changamoto hizo Ofisi
ya Makamu wa Rais inatambua mchango wenu katika shughuli za udhibiti
na usimamizi wa taka hatarishi ikiwemo taka za kielekitroniki na
tunafahamu kabisa dunia yote kwa sasa inaelekea kwenye uchumi wa
mzunguko ambao kwa lugha rahisi tunaweza kuuita “taka ni mali”
(circular economy), kwa hiyo ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli
za uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ni muhimu sana.
Akiongea katika Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuwa Mkutano huo una lengo la kujua changamoto zinazowakuta wadau wa biashara hiyo.
Naye mmoja wa Wafanyabiashara hao kutoka Gaia Industry Bi Rehema Ally, ametoa maoni kuwa mchakato wa vibali vya taka hayarishi uanze kufanyika mtandaoni (online). Katika suala hilo Waziri Jafo ametoa maagizo kwa NEMC kuwa katika siku 45 mchakato huo wa mtandaoni uwe tayari umekamilika na kuwezesha Wadau kutumia mfumo huo.
Post A Comment: