Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuwasilisha mashahidi.

Kesi hiyo ya jinai namba 66 ya mwaka huu,iliyopangwa kuanza kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi  huku upande wa Jamhuri kushindwa kuwaleta mashahidi mahakamani ambapo Wakili wa Serikali Trasila Asenga aliomba mahakama hiyo kupewa tarehe nyingine ya kusikilizwa kwa kesi hiyo kutokana na shahidi waliyemtegemea mahakamani kutoa ushahidi kupatwa na udhuru.


Lengai Ole Sabaya na wenzake saba wanawakilishwa na mawakili wao wakiongozwa na Wakili Dankan Owora na Wakili Mosses Mahuna.


Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Hakimu Salome Mshasha aliahirisha kesi hadi Julai 16 mwaka huu.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI KUTOKA MAHAKAMANI











Share To:

Post A Comment: