Mkuu wa Mkoa Iringa,  Queen Sendiga ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Tumaini Festival litakalofanyika katika ukumbi wa Royal Palm, Mjini Iringa.
Msanii Hafsa Kazinje ambaye ni miongoni wa wanamziki atakayetoa burudani kwenye tamasha hilo
Msanii Mess Chengula atakuwepo kutoa burudani kwenye tamasha hilo
 


Na Mwandishi Wetu, Iringa


MKUU wa Mkoa wa Iringa,  Queen Sendiga anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Tumaini Festival litakalofanyika katika ukumbi wa Royal Palm, Mjini Iringa.

Tamasha hilo lililoandaliwa na mwimbaji wa muziki wa Injili, Dkt.Tumaini Msowoya ambaye pia ni mwanahabari, linalenga kufanya uzinduzi wa albamu yake mpya inayoitwa Mwamba.

Pamoja na kiongozi huyo wa mkoa, viongozi mbalimbali wakiwamo wabunge, wakurugenzi na Mkuu wa Wilaya y Iringa, wameahidi kuhudhuria tamasha hilo.

Akizungumza na wanahabari Iringa, Msowoya alisema tamasha hilo litakutanisha wasanii wengi kutoka nje na ndani ya mkoa wa Iringa.

“Nawaomba wakazi wa Moa wa Iringa nan je kuhudhuria tamasha hili la aina yake,” alisema Dkt. Msowoya.

Aliwataja baadhi ya wasanii watakaopamba tamasha hilo kuwa ni Hafsa Kazinje, Mess Chengula na wengine wengi.

Share To:

Post A Comment: