-Kusikiliza kero za Wananchi baada ya bunge


Na Andrew Chale.


MBUNGE wa Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga 'Senator  Sanga' kuanza ziara maalum ya Kata hadi Kata katika Vijiji vya Jimbo hilo ili kutatua, kushukuru, kusikiliza kero na kushiriki kazi za maendeleo baada ya hivi karibuni kuhitimisha Bunge la Bajeti.Mhe. Senetor Sanga amesema baada ya kuhitimisha bunge la bajeti 30 Juni mwaka huu,  ameona ni wakati sasa wa kurejea tena kwa Wananchi.


"Baada ya kuwasilisha mawazo ya wananchi Bungeni na kuomba walivyonituma, Niombe sasa ni muda wa kurejea  tena kwao kutatua, kushukuru, kusikiliza kero na kushiriki kazi za maendeleo.


Tunaanzia Kata ya Lupalilo, Iwawa, Bulongwa, Tandala, Luvumbu  ni mwendo wa kijiji kwa kijiji kuanzia tarehe 8-17 Julai 2021" Alibainisha.


Ambapo aliongeza kuwa, Mkutano wa kwanza unatarajiwa kufanyika 8 Julai mwaka huu majira ya saa Saba mchana   eneo la Tandala Mjini.


12 Julai mikutano itafanyika Ihela, Ikonda na Usagatikwa huku 13 Julai itakuwa Lupalilo katika Vijiji vya Kisinga, Mago, Lupalilo, Ilevelo na Ugabwa.


Pia mikutano mingine ni 14 Julai mkutano utakuwa Iwawa katika Vijiji vya Maleutsi, Ludihani, Ndulamo, Ivalalila na Iwawa huku 15 Julai ni Luwumbu katika Vijiji vya Uganga, Luwumbu, Lugao, Unenamwa na Usililo.


Aidha, 16 Julai, Kata ya Bulongwa mikutano itakuwa Vijiji vya Utanziwa, Imehe, Ilolo, Idende, Bulongwa na mwisho atahitimisha 17 Julai, mkutano utafanyika Iniho  katika Vijiji vya Unyangogo, Mwakavuta, Lumage, Kidope na Iniho.


Aidha, Mhe. Sanga amekuwa mstari wa mbele katika kutanguliza maslai ya umma haswa wananchi wake amekuwa akiwasilisha kero mbalimbali Bungeni katika kutatua ambapo pia ameshashughulikia kero za maji safi na salama, Umeme, Miundombinu na mengine mengi ikiwemo kushirikina na wananchi wa jimbo katika shughuli za kijamii.


Mwisho.

Share To:

Post A Comment: