Na Mwandishi wetu,Mbeya


KAMPENI  iliyoanzishwa na Madiwani wa Viti Maalum Jiji la Mbeya ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika Shule ya Msingi Kambarage iliyopo Kata ya Ruanda Jijini Mbeya imeendelea kushika kasi baada ya kuungwa mkono na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye ameshirikiana na madiwani hao na kukabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo.


Akikabidhi saruji hiyo Naibu Meya wa Jiji la Mbeya , Agnes Mangasila kwa niaba ya Madiwani na Mbunge alisema ili kuwa msaada huo utasaidia kutatua msongamano wa watoto wanapokwenda katika maliwato kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi.


Ramadhani Tamimu ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Soweto kwa niaba ya wananchi ameshukuru kupokea msaada wa saruji na kwamba matundu ya vyoo yatakamilika kwa wakati.


Naye Mtendaji Kata ya Ruanda , Faraja Msuwila mbali ya kumshukuru Naibu Waziri wa Maji pia ameshukuru Madiwani kwa moyo wa kujitolea ili kuwaondolea changamoto wanafunzi wa shule hiyo.


Zoezi la kutoa saruji limeanzia shule ya Msingi Mponja ambapo kwa umoja wao Madiwani na Naibu waziri wa maji Mhandisi Mahundi walitoa mifuko kumi ili kuendeleza ujenzi wa matundu ya vyoo vya wasichana.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: