Mmoja ya mwanachama wa UDI Hassain Imamu akimkabidhi kitabu mkuu wa wilaya ya lushoto Kalisti Lazaro.

Wana-UDI wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya Kalisti Lazaro mara baada ya kufungua mkutano wao mkuu wa mwaka
Mkuu wa wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro (aliyevaa kofia)  akifurahia jambo pamoja na viongozi wa UDI. Kulia kwa mkuu wa wilaya ni Katibu wa CCM wilaya Ramadhani Mahanyu, ofisa wa UDI na kulia ni Ali Daffa
Mwenyekiti wa UDI Ali Daffa akimkabidhi kofia na t-shirt mkuu wa wilaya kama ishara ya kumkaribisha katika wilaya hiyo


UMOJA wa Maendeleo wa Usambara (UDI),  umesema utamuunga mkono Mkuu mpya wa Wilaya ya Lushoto, Kalisti Lazaro ili kuharakisha maendelea ya wilaya hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa umoja huo wa Usambara Development Initiative (UDI) mwenyekiti wa umoja huo Ali Daffa alisema wamefurahishwa na hatua nzuri ya mashirikiano baina ya umoja huo na serikali.

Daffa alimshukuru kwa kukubali wito wao wa kuja kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa UDI na kumhaidi kumpa ushirikiano katika shughuli za kuwalete Wananchi wa Lushoto Maendeleo.

"Kiukweli mkuu wa wilaya tumefurahishwa na mashirikiano uliyoyaonesha kwetu tumekualika muda mfupi sana umekuja lakini umeaahidi tutakuwa pamoja katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Lushoto na sisi tunakuaahidi tutakuwa na wewe bega kwa bega kuhakikisha tunafanya kazi pamoja, " alisema Daffa.

Umoja huo wenye zaidi ya wanachama 150 waliopo ndani na nje ya nchi, umekuwa ukisaidia kutatua changamoto mbalimbali wilaya hiyo katika huduma za jamii.

Umoja huo ambao unajumuisha Wadau wa Maendeleo kutoka maeneo ya Usambara (Lushoto, Mlao, Bumbuli) wanaoishi maeneo mbalimbali ya Nchi na Nje ya Nchi, umekuwa mahususi kushughulikia changamoto za wananchi ikiwemo kukarabati shule za wilaya hiyo.

Umoja huu umekuwa ukisaidia Jamii ya watu wa Lushoto katika Njanja mbalimbali za Maendeleo kama kuboresha huduma za jamii, ukarabati wa shule, uboreshaji wa huduma za afya.

Akizungumza katika mkutano huo,  Mkuu wa Wilaya amewapongeza viongozi na wanachama wa UDI na kuhaidi kuwapa ushirikiano wa dhati katika kuwaletea Wananchi wa Lushoto Maendeleo.

Pia aliwaasa wana UDI kudumishi umoja, mshikamano, upendo na kutobaguana kwa itikadi za kisiasa, dini na ukabila.

Pia Wana UDI walimzawadia Mkuu wa Wilaya zawadi ya Kofia na Tshirt ambazo zimekuwa na nembo ya UDI pamoja na kumpa kitabu cha Dhahabu ya Amani.
Share To:

Post A Comment: