Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiupongeza mkakati ulioandaliwa kwa lengo la kusaidia kuvitangaza vivutio vya utalii vya kusini mwa Tanzania
Baadhi ya wadau wa utalii waliohudhulia kwenye mkakati wa kuhakikisha wanavitangaza vivutio vya kitalii vya kusini mwa Tanzania
Picha ya pamoja ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga na wadau wa utalii kusini mwa Tanzania.

 
 
Na Fredy Mgunda,Iringa.

MKUU wa mkoa wa Iringa amepongeza mikakati ya bodi ya utalii (TTB) ya kutangaza vivutio vya kitalii vilivyopo kusini mwa Tanzania ambavyo vitachochea kukuza uchumi wan chi na kuleta maendeleo kwa ujumla.

Akizungumza kwenye kikao cha mikakati ya kutangaza vivutio hivyo, Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga alisemakuwa bodi ya utalii imejitahidi kwa kiasi kikubwa wametangaza vivutio vya kusini mwa Tanzania kwa njia mbalimbali ikiwa ndani ya nchi hadi nje ya nchi ambako wameongeza watalii kwa kiasi kikubwa.

Alisema kuwa TTB kwa ushirikiano na wadau wa utalii wanatakiwa kuendelea kuvitangaza vivutio hivyo kwa kasi kubwa ili kukuza vipato vya wananchi na kukuza pato la taifa na kuchangia maendeleo ya nchi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati na ile ambayo imebuniwa na watalaam.

Sendiga aliiomba bodi ya Utalii (TTB) kuendelea kuongeza mikakati ya kuvitangaza vivutio vilivyopo kusini mwa Tanzania kwa kuwa bado kuna vivutio vya kitalii vingi havijatangazwa kama inavyotakiwa kama ambavyo vinatangazwa vivutio vingine.

Alisema kuwa mkoa wa Iringa ni mmoja ya mkoa ambao unavivutio vingi na unafikika kwa kirahisi hivyo kuendelea kuvitangaza vivutio hivyo vitachangia kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa kwa kasi kubwa na kupokea watalii wengi.

Sendiga aliwaomba wadau wa maswala ya utalii kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya barabara,huduma bora za hotel kwa lengo la kuwavutia watalii wengi kuja mkoani Iringa kwa kuwa kunavivutio vingi ambavyo kwa kiasi kikubwa kunasaidia kukuza pato la nchi.

Kwa upande wake kaimu meneja wa mikutano na matukio kutoka bodi ya utalii Tanzani,Irene Mvile alisema kuwa wadau wa utalii kwa kushirikiana na serikali kwa pamoja wanaweza kutekeleza mkakati huo wa kukuza utalii wa kusini mwa Tanzania na kukuza pato la taifa kwa ujumla kwa kuongeza idadi kubwa ya watalii kutembelea vivutio vilivyopo.

Alisema kuwa wadau wa kusini ndio wanajua vivutio vilivyopo kusini mwa Tanzania na namna ya kuvitangaza hivyo wadau wanapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa serikali ili kufanikisha kuvitangaza vivutio vilivyopo.

Aliongeza kwa hivi sasa wapo na wataalam wa kusaidia kuvitangaza vivutio vilivyopo kusini mwa Tanzania kwa kuanza kutoa semina kwa wadau wa  utalii wa kusini mwa Tanzania ili wajue namna ya kuwavutia watalii na kuvitangaza vivutio vilivyopo.

MWISHOO.

Share To:

Post A Comment: