Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.
 
Pia, mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja akitakiwa kutokujihusisha makosa yoyote ya jinai.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa Sh200 milioni benki na kiasi kinachobakia anatakiwa kukilipa ndani ya mwaka mmoja kuanzia siku ilipotolewa hukumu.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 16, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa makubaliano ya kuimaliza kesi hiyo.
 
Awali, mawakili wawili wakuu wa Serikali, Marterus Marandu, Renartus Mkude na wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon na Faraja Ngukah, walidai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka yake baada ya kuingia makubaliano na DPP..

Katika kesi ya msingi, Seth anadaiwa kati ya Novemba 29, 2013 na Januari 24, 2014 katika benki ya Stanbic na benki ya Mkombozi iliyopo  Wilaya ya Ilala na mwenzake James Rugemalira walijipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.
Share To:

Post A Comment: