Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai, *Mchungaji James Kalekwa* wa New vine Church (NVC) Dodoma ameandaa zawadi ya vitabu 20 vya kieletroniki (eBooks) kwa watu wote. 

 Zawadi hiyo itatolewa kuanzia *tarehe 20 Juni*, 2021 (Saa 6:1 Usiku). Akizungumza wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la New Vine Church lililopo Jijini Dodoma, Mchungaji James Kalekwa amesema lengo la kutoa vitabu hivyo ni watu waweze kujisomea ili wapate ufahamu wa neno la MUNGU lakini pia vitabu hivyo itakuwa ni zawadi yake kwa watu wote katika siku yake muhimu yakusherekea siku ya kuzaliwa kwake. 

"Na atukuzwe Mungu kwa zawadi ya uhai. Tunapewa zawadi ya uhai ili tuutumie kuwa zawadi kwa wengine. Ni kwa sababu hii ndiyo nilipewa zawadi ya uhai... ili niujaze ulimwengu kwa maarifa ya utukufu wa Mungu kama maji yaifunikavyo bahari." alisema Mchungaji James Kalekwa. 

Vitabu hivyo ni pamoja na: 📘 *Mahusiano 101* 📕 *Mahusiano 102* 📗 *Mahusiano 103* 📙 *Imeandikwa* 📘 *Kuomba NENO la Mungu* 📙 *NYWILA* 📕 *Kukaa Chini ya Malezi na Unasihi* 📗 *Kuhusiana na Watu kwa Mipaka* 📕 *Acha Wafu Wawazike Wafu Wao* 📘 *Ibada ya Sifa* 📙 *Ufuasi* 📗 *Neema ya Ufuasi Imefunuliwa Kwetu* 📕 *Jizoeze Kupokea Maonyo kwa Furaha* 📘 *Tafakari zangu kuhusu NEHEMIA - 1* 📕 *Ni Maandiko au Neno?* 📗 *Masumbufu ya Maisha* 📙 *Mimi ni Mwanamume* 📘 *Mlima wa Elimu* 📕 *Mlima wa Habari na Mvumo wa Injili* 📗 *Mfuasi Mfano wa Epafradito* 📙 *Sisi ni Watu wa Mlima Sayuni* na 📘 *Lakini MUNGU* 

Aidha, Pst. James Kalekwa amesema kuwa wakazi wote nchini wanaweza kupakua vitabu hivyo kwa njia ya mtandao ambavyo vitapatikana siku ya tarehe 20 Juni, 2021. "Unaweza kupata nakala ya vitabu hivi kwa njia mbalimbali: 

1. Jiunge na group la WhatsApp la kupokea na kusambaza vitabu kwa link hii (ni group la muda tu June 20-July 20). 👇 https://chat.whatsapp.com/HTdG9bIZqRtBkpKvjQ1j0G 2. Vitabu vyote vitapatikana kwenye maktaba ya mafundisho ya New Vine Church - Dodoma, *Telegram.*👇 https://t.me/nvcdodoma 3.

Wasiliana na mwandishi moja kwa moja kwa *0754-917-765*/Facebook: *James Kalekwa*/IG: *james_kalekwa*," alisema Mchunjaji Kalekwa. Mchungaji Kalekwa ametoa rai kwa wasomaji watakao hudumiwa na vitabu hivyo kuhakikisha wanawapatia watu wengine link ya vitabu hivyo ili wasome na wahudumiwe bila malipo.

 

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: