Muasisi wa Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, Flaviana Matata akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Eatv Regina Mengi mara baada ya kutia saini makubaliano ya ushirikiano kwa ajili ya kampeni ya Namthamini nasimama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Eatv Regina Mengi wakikabidhiana mkataba na muasisi wa Taasisi ya Flaviana Matata Foundation baada ya kutia saini makubaliano ya ushirikiano kwa ajili ya kampeni ya "Namthamini nasimama naye "katika kuhakikisha upatikanaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wakike nchini.


 Na Khadija Seif

MWANAMITINDO nchini ambaye pia ni mdau mkubwa wa Vijana hususani wasichana kwenye afya ya uzazi na hedhi salama  Flaviana Matata ametia saini ya makubaliano ya ushirikiano kwa ajili ya Kampeni ya 'Namthamini' ya kituo cha redio pamoja na Televisheni cha East Africa nchini.

Akizungumza na Michuzi Tv Mara baada ya utiaji saini Mkurugenzi Mtendaji wa Eatv Regina Mengi amesema Mwanamitindo huyo ataweza kusaidia vijana pamoja na kuhamasisha Hedhi Salama kwa vijana hususani mashuleni,vyuoni na hata mitaani.

"Matata ni Miongoni mwa Wasichana wakitanzania wenye nyia ya kusaidia wasichana wadogo ambao wanapitia changamoto ya kutoweza kumudu kununua taulo za kike , hivyo tumeona ipo haja ya kumteua na kusaini nae mkataba wa kutangaza kampeni yetu ya "Namthamini nasimama nae" yenye lengo la kuhamasisha kusaidia watoto wakike mashuleni na kuwapatia taulo hizo za kujikinga."

Pia Mengi ameeleza kampeni hiyo iliyozinduliwa mwaka 2017 imeweza kuleta manufaa na ndio sababu ya kuona ipo haja ya kuendeleza mapambano ya Kampeni hiyo.

"Kwa mwaka 2017 tuliweza kuwafikia wanafunzi elfu 11, tunaomba watanzania wote Kushirikiana nasi pamoja na Mdau wetu mpya kabisa Flaviana kuongeza nguvu ya upatikanaji wa taulo za kike."

Nae Mwanamitindo Flaviana Matata ametoa pongezi na shukrani kwa Kituo hicho cha televisheni pamoja na Redio kwa kumpa Mkataba wa kushirikiana na vijana kuhakikisha taulo za kike kwa Wasichana zinawafikia kwa wepesi na kwa nafuu kupitia Kampuni yake ya Flaviana Matata Foundation yenye kutengeneza pedi aina ya "Lavy".

"Tunajua changamoto ni nyingi zinazomzuia Mtoto wa kike kwenda shule kutokana na kutomudu gharama za taulo za kike na kwa kushirikiana na Kampeni ya "Namthamini "tunaomba tuhaidi kuweka mkakati wa kufikia watoto wakike takribani elfu 5 ili waweze kubaki mashuleni wakiwa huru na salama kutokana na uwepo wa taulo za kike inayomfanya awe kujikinga."

Hata hivyo Matata amehimiza Watu maarufu na wenye mchango kwenye jamii akimtaja Mkurugenzi wa clouds Media pamoja na Msanii Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz kuwekeza nguvu kwenye kusaidia watoto wakike mashuleni katika kuwapa taulo za kike.

"Napenda kuwapa nafasi Watu wa habari nategemea Kaka yangu Joseph Kusaga ,Majizo pamoja na Diamond wataweza kuweka nguvu kwenye hili na sio peke yangu tu nategemea kuungwa Mkono ili kuleta nguvu kubwa na msukumo wakusaidia watoto wakike."

Share To:

Post A Comment: