Na Leylah Nassib - DSJ 

MTANGAZAJI  wa kipindi cha Mashamsham kinachorushwa Wasafi FM, Khadija Isihaka Shaibu maarufu kama Didah jioni ya jana amefunga ndoa na Diwani wa  Vingunguti na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto.

Ndoa hiyo imekuja baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu kufuatia na mbwembwe nyingi za baadhi ya wasanii na wafanyabiashara kuahidi pesa ndefu za kutoa katika harusi hiyo ambapo wasanii na waigizaji wakiwemo Diamond platnumz, Rayvanny, Mbosso, Irene Uwoya, Aunt Ezekiel na wengine wengi walihaidi kutoa pesa nyingi ili kufanikisha shughuli hiyo.

 Ndoa hiyo ilifanyika Sinza nyumbani kwa akina Didah, na kupitia ukurasa wake wa Instagram Didah ameweka video na kuchapisha ujumbe ujumbe wa kuthibitisha tayari amekuwa mke wa mtu na ametoa shukurani zake za dhati kwa Mama Diamond 'Mama dangote' na Mumewe Uncle Shamte pamoja na Dada wa diamond Esma platnumz pamoja na watangazaji wenzake wa Wasafi Media na kuwaalika kuhudhuria sherehe zaidi ya ndoa hiyo leo katika ukumbi wa Escape One. 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: